Anza wikiendi na filamu hii mpya

Rodgers George 0744Hrs   Oktoba 11, 2019 Maoni & Uchambuzi

Kutana na msanii Will Smith ambaye hadi kutoka kwa filamu ya Gemini Man ametimiza filamu ya tatu kumhusisha kwa mwaka 2019. picha| Mtandao.


  • Fikiria kuangalia Gemini Man ya Will Smith iliyotoka hivi karibuni.
  • Ngumi pekee siyo utakazojionea kwani imejaa mafunzo lukuki yakiwemo umakini katika kila ufanyalo.

Dar es Salaam. Ile filamu ambayo iliyokuwa inasubiriwa kutoka mwisho wa mwaka huu tayari ipo kwenye kumbi za kuangalizia sinema zikiwa zimebaki siku 82 kuingia mwaka 2020.

Filamu hiyo ni Gemini Man ambayo ni miongoni mwa filamu tano ambazo zinakusudiwa kutoka kabla ya mwaka huu kuisha. Filamu nyingine ni Jumanji The Next level, Frozen II, Cats na Star Wars, The rise of Skywalker.

Kutana na msanii Will Smith ambaye hadi kutoka kwa filamu ya Gemini Man ametimiza filamu ya tatu kumhusisha kwa mwaka 2019.

Katika filamu ya Gemini Man ni ngumi na mateke na vurugu zinazomwelezea Smith, anayeigiza kama Henry Brogan.

Brogan ambaye ni muuaji anayegeuka kuwa mlengwa wa muuaji ambaye ni mdogo zaidi na mwenye kasi ambaye kwake (Henry) hafui dafu.

Hata hivyo, Henry anapatwa na mshangao pale anapogundua kuwa muuaji  ni  mtu anayefanana naye wakati akiwa mdogo. 


Zinazohusiana


Unaachaje kumfuatilia Smith ambaye ameigiza filamu takribani 50?. Fuatilia mkasa huu ulioongozwa na Ang Lee anayeshikilia tuzo zaidi ya 30 za uongozaji filamu ambaye pia ni kichwa nyuma ya filamu kama Hulk ya mwaka 2003

Ndani ya siku saba zijazo kuanzia leo, tembelea kumbi za kuangalizia sinema zikiwemo Mlimani City na Aura Mall huku ukikaa mkao wa kula kwa filamu zingine zinazokuja zikiwemo za Jumanji Next level, Frozen na Cats.

Related Post