Filamu ya “The Love Birds” inakusubiria kuipamba wikiendi yako

May 22, 2020 9:48 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayohusu wapenzi wawili wanaolazimika kuanza safari ya kusaka mhalifu aliyechafua majina yao.
  • Mhalifu huyo aliyeua na kuwakimbia, amewaweka wawili hao kwenye rada za polisi.

Dar es Salaam. Muziki wa bendi ya zamani ya “Foreigner”  wa “I wanna know what love is” ni sahihi kwa wawili hawa ambao penzi lao lipo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.

Vicheko vya kuoneana aibu na matembezi ya kudumisha mahusiano vinaendelea kuchagiza penzi la Kumail Nanjiani na binti mwenye ngozi yake, Issa Rae.

Hata hivyo, safari inabadilika ghafla baada ya wawili hao kupata ajali na kumgonga abiria aliyekuwa akiendesha baiskeli.

Usiogope! Hakuumia, alinyanyuka na kuendelea na safari. 

“Mimi ni askari huyo ni mhalifu, sogea sogeaa!” ni sauti inayotoka kwa jamaa mmoja nje ya gari lakini baada ya polisi huyo kuingia ndani, anafumkuzia mwendesha baiskeli na kumgonga na kisha kuhakikisha amemuua.

“Sidhani kama ni polisi,” anasema Nanjiani akimwambia mpenzi wake anayetikisa kichwa kuashiria anasadiki.


Zinazohusiana


Hata hivyo, wawili hao wamechelewa kwani jambazi aliyejiita polisi, ameondoka na sasa mashaidi wamewaona na kudhani wao ndio wauwaji.

Unapenda filamu za “action” wewe? Hapa ndipo inapoanzia. Wawili hao wanaanza safari ya kumtafuta jambazi huyo ili wasafishe majina yao kwani wanatafutwa na polisi.

Kuvamia shughuli za watu, kukosea nyumba, kupiga watu wasio na hatia ni kati ya misukosuko wanayopitia wapenzi hao wakati wanatafuta furaha ya milele kwenye penzi lao.

Filamu hiyo imepanda kwenye mtandao wa Netfllix leo saa sita na dakika 19 mchana hivyo bado mpya.

Umevutiwa? Unachohitaji ni App ya Netflix iliyolipiwa kutazama filamu hiyo ya “Love Birds” inayochukua saa moja na nusu huku ikifaa watu wenye umri wa miaka 16 na zaidi.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

Nukta TV

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV