Fedha za Uviko-19 kununua magari 195 ya wagonjwa Tanzania

June 9, 2022 10:03 am · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kati ya Sh1.3 trilioni zilizotolewa na IMF kupambana na Uviko-19.
  • Halmashauri zote nchini kupata magari hayo.
  • Wabunge waanza kuyaomba kabla hayajanunuliwa.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imepanga kununua magari ya wagonjwa 195 kutoka katika fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kukabiliana na athari za kijamii na kiuchumi za Uviko-19 ili kurahisisha huduma katika vituo vya afya.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dk Festo Dugange amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo (Juni 9, 2022) wakati wa kipindi cha maswali na majibu huku akisisitiza kuwa baada ya ununuzi wa magari hayo halmashauri ndiyo zitafanya tathimini ya uhitaji wa magari ya wagonjwa kupelekwa katika vituo cha afya.

“Ni maamuzi ya halmashauri kuona kipaumbele kwa wakati huo, gari hilo litakwenda katika kituo cha afya au kwenye hospitali ya halmashauri,” amesema Dk Dugange

Huenda idadi hiyo ya magari yanayotarajiwa kununuliwa ikaongezeka kwa kuwa Serikali ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) katika ununuzi wa magari hayo.


Soma zaidi: 


Tanzania ina jumla ya halmashauri 184 ambapo katika mpango huo wa ununuzi wa  magari hayo yanayotumiwa kubeba wagonjwa hasa wakati wa dharura, ugawaji utazingatia maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Septemba 2021, Shirika la Fedha Duniani (IMF) liliidhinisha kuipatia Tanzania mkopo wa dharura wa Dola za Marekani milioni 567.25 (Sh1.3 trilioni) kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa Corona (Uviko-19).

Fedha hizo zilizotolewa na IMF zinatumika ndani ya miezi tisa kuimarisha sekta elimu, maji na afya kwa kuongeza kasi ya utoaji chanjo ya Uviko-19,  uboreshaji wa sera za fedha ili kuendana na hali ya wakati huu na kuinua sekta isiyo rasmi ambayo imeajiri Watanzania wengi.

Wabunge wayaomba magari hayo

Baadhi ya wabunge wameomba Serikali kupeleka magari hayo kwenye majimbo wanayotokea kutokana na uwepo wa uhaba wa magari ya wagonjwa.

“Kutokana na ukubwa na upekee wa hospitali ya Kawe iliyokuwa Mabwepande, hamdhani kwamba (Serikali) jimbo la kawe linatakiwa kupata gari kwa upekee?,” ameuliza Halima Mdee, Mbunge wa Viti Maalumu

Naye Boniphace Butondo, Mbunge wa Kishapu amesema “ninaomba kuletewa gari na lipelekwe katika tarafa ya Mondo ambayo itaongeza uwepo wa magari kwenye tarafa hiyo.”

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV