Dk Biteko awataka Makatibu Mahsusi kujiendeleza kitaaluma

May 23, 2024 3:26 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema kujiendeleza kitaaluma kutawawezesha kuendaana mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Mwanza. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametoa wito kwa makatibu mahsusi nchini  kujiendeleza kitaaluma ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia sambamba na kuboresha utendaji kazi wao.

Dk Biteko aliyemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa 11 wa kitaaluma wa Makatibu Mahsusi leo Mei 23, 2024 jijini Mwanza amesema ni ngumu kwa watumishi hao kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia bila kuwa na elimu.

“Kama mnavyofahamu kuwa dunia ya leo ni kijiji kutokana na mabadiliko ya teknolojia na utandawazi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochea maendeleo ya teknolojia hususan Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)…

…Hivyo ni jukumu lenu kama chama cha kitaaluma kuwa na mkakati  wa kushawishiana kujiendeleza kitaaluma kwenda sambamba na mabadiliko hayo” amesema Dk Biteko.


Soma zaidi:Viwanja Afcon vyaongeza bajeti ya michezo mara nane Tanzania


Amesema mfumo wa kisasa wa matumizi ya kompyuta na vishikwambi ambao kwa pamoja unarahisisha utendaji kazi zao na ni jukumu lao kama waandishi waendesha ofisi kuhakikisha kuwa wanabobea katika fani hii na matumizi ya  vifaa hivi kwenye kada yao.

DK Biteko pia  amewataka makatibu mahususi hao kusaidia wengine katika kutatua changamoto mbalimbali katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kuwa Serikali imefanya maboresho kadhaa katika kada ya makatibu mahsusi kwa lengo la kuboresha taaluma hiyo nchini.

“Mwanzoni kabisa taaluma hii ilikuwa inaitwa uhazili na kada yao hawa walikuwa wanaitwa makatibu mahsusi, tangu mwaka jana muundo umebadilika na sasa kwa kada yao wanaitwa waandishi waendesha ofisi  na kiutumishi wamepanda  kwa ngazi ya mshahara hadi kufikia TGSH hivyo maafisa hawa sasa wanasoma kufikia shahada hadi ngazi ya ubobevu,” amesema Simbachawene.

Makatibu Mahsusi wakiwa kwenye mkutano wa pamoja uliofanyika Jijini Mwanza. Picha na Mariam John/ Nukta

Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga amesema lengo la mkutano huo ni kudumisha taaluma, kukuza uwajibikaji, kuipa hadhi taaluma yao, kuboresha maslahi yao pamoja na kutoa huduma bora kwa waajiri na wananchi.

Ametaja baadhi ya mafanikio ya chama hicho kuwa ni kuishawishi Serikali kuanzisha shahada ya uzamili katika Chuo cha Uhazili Tabora na Chuo cha Utumishi wa Umma pamoja na kuboresha muundo wa maendeleo wa kada ya waandishi waendesha ofisi hadi kufikia daraja la afisa mwendesha ofisi mkuu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV