Corona: Serikali ya Tanzania haijatangaza kufunga shule, vyuo

July 1, 2021 10:04 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya watu wanapotoshwa kwa kusambaza habari ya mwaka jana.
  • Habari hiyo ni ya tangazo la kufunga shule na vyuo Aprili 2020.
  • Serikali haijafunga shule wala vyuo kwa sababu ya Corona.

Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni mwa watu waliopata video fupi kwenye mitandao ya kijamii inayosema Serikali imefunga shule na vyuo kuwakinga wanafunzi na Corona, fahamu kuwa ni uzushi. 

Licha ya kuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wako likizo, Serikali haijatoa tamko lolote la kuzifunga shule hizo kipindi hiki.

Habari hiyo ambayo iko kwenye mfumo wa video inamuonyesha mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV, Farhia Middle akitoa habari kuwa Serikali imefunga shule na vyuo kuwakinga wanafunzi na Corona.

Pia video hiyo ambayo inasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa tangazo hilo.

“Shule zote na vyuo kuendelea kufungwa kwa tahadhari ya Corona hadi serikali itakapotoa tamko jingine,” inaeleza sehemu ya habari hiyo.

Nje, ndani ya habari hiyo

Uchunguzi uliofanywa na timu ya Nukta Fakti kwa kutumia zana za kidijitali ikiwemo TinEye umebaini kuwa taarifa hiyo ni ya kweli lakini ilitolewa na Serikali Aprili 2020 na ITV ilichapishwa katika mtandao wake wa Facebook.

Majaliwa  alitoa tamko hilo katika kikao cha kitaifa cha uratibu wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona jijini Dodoma mwaka jana na siyo mwaka huu kama inavyosambazwa na wapotoshaji.

Wanafunzi na walimu ambao shule zao zinafunguliwa kuanzia Julai 5, 2021 wametakiwa kuipuuza habari hiyo na kuendelea na maandalizi ya kuingia muhula wa pili wa masomo.

Ili kupata taarifa sahihi za Corona, Watanzania wanashauriwa kutumia vyanzo sahihi ikiwemo Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO)

Pia kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyosisitiza, wanashauriwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na kuepuka misongamano isiyo ya lazima. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV