Corona: Chanjo ya Abdala haibagui jinsia

June 23, 2021 1:21 pm · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakuna chanjo inayoitwa Abdallah bali ipo inayoitwa Abdala kutoka nchini Cuba.
  • Hakuna taarifa zozote zinazoonyesha kuwa chanjo ya Abdala inawafaa wanawake.

Dar es Salaam. Habari  inayosambaa katika makundi ya WhatsApp nchini Tanzania ikiwa na picha za chupa za chanjo ya aina ya  Abdala ni ya kutiliwa mashaka kwa sababu habari hiyo ya uzushi imesema inafaa zaidi wanawake.

Picha hiyo imeambatana na maelezo katika lugha ya Kiswahili yanayodai “Hii Chanjo ya Abdallah ndo yawafaa Wanawake”.

Ukweli uko wapi?
Habari hiyo ni ya kutilia mashaka  kwa sababu ina upotoshaji ndani yake hakuna chanjo inayoitwa Abdallah kama ilivyoelezwa na mtoa taarifa bali kuna chanjo aina ya Abdala ambayo imetengenezwa nchini Cuba.


Chanjo ya Abdala ambayo imethibitishwa hivi karibuni na Cuba ikiwa katika  awamu ya tatu ya majaribio yake kuwa na ufanisi wa asilimia 92.3 kama mtu atafanikiwa kupata dozi zote tatu za chanjo hiyo.


Chanjo hiyo imetengenezwa nchini Cuba na taasisi mbili za Center for Genetic Engineering and Biotechnology of Cuba ambapo  Februari 1, 2021 ilianza kufanyiwa majaribio ya awamu ya pili.
Chanjo hiyo ni ya pili kutangazwa nchini humo baada ya  Soberana 2, chanjo ambayo ufanisi wake ni asilimia 62 kwa dozi mbili tu kati ya tatu.


Chanjo zote mbili zinatarajiwa kuidhinishwa kwa matumizi ya dharura siku chache zijazo na mamlaka nchini humo.Cuba ambayo hadi Juni 23, 2021 imeripoti  kesi 170,854 za Corona na vifo 1,180 imekataa kuagiza chanjo za nje badala yake itatumia chanjo ambazo imetengeneza yenyewe.

Inafaa wanawake pekee?
Tofauti na maelezo ya uzushi uliotolewa katika picha hiyo hapo juu, maelezo yaliyotelewa na  watengenezaji wa chanjo hiyo ni kuwa   chanjo hiyo  inalenga watu wa jinsi zote .

 
Hata hivyo, chanzo zote za Corona ambazo zimeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) hakuna hata moja ambayo inabagua wanawake au wanaume. Kwa hiyo madai ya anayesambaza habari hiyo hayana mashiko kwa sababu chanjo za Corona hazibagui jinsia fulani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV