Chadema kuanza wiki ya maandamano nchi nzima

March 7, 2024 1:19 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Maandamano hayo yatafanyika Aprili 22 hadi 30 mwaka huu.
  • Wanachama wake katika maeneo mengine duniani kuandamana katika nchi zao.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuanza kwa  wiki ya maandamano yatakayofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 30 Aprili 2024 katika makao makuu ya chama hicho nchi nzima.

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 6, 2024 mkoani Mtwara amesema uamuzi huo umetokana na Serikali kupuuzia maandano yaliyopita na hali ngumu ya maisha iliyopo nchini.

“Kwa vile Serikali imekataa mabadiliko ambayo Watanzania wameyataka kwa nia za mazungumzo na maridhiano sasa Watanzania watayapata mabadiliko hayo kwa njia ya nguvu ya umma na njia nyingine za shinikizo kama maandamano, migomo na njia nyingine,” amesema Mbowe.

Aidha kiongozi huyo amewataka wananchama wa Chadema waliopo katika maeneo mengine duniani kuandamana katika miji yao ili kufikisha ujumbe wa hali iliyopo nchini Tanzania.

Maamuzi hayo ya wiki ya maandamano yanayofanyika na Chadema ni sehemu ya azimio lilioandaliwa na kamati kuu ya chama hicho iliyokutana kwa kuanzia Machi 4 hadi Machi 6 mkoani Mtwara.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
18 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
18 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
18 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Nukta TV

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV