Bunge lapitisha bajeti ya 2020-21, tozo matangazo kwenye magari zikipunguzwa

June 15, 2020 11:20 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bajeti hiyo ya Sh34.88 trilioni imepita baada ya wabunge 304 kupiga kura za ndiyo huku wabunge 63 wakipiga kura za hapana.
  • Itapunguza kutoka kiwango cha sasa cha Sh10,000 hadi Sh4,000. 
  • Lengo ni kuongeza kasi ya wafanyabiashara kutangaza ili kuipatia Serikali mapato. 

Dar es Salaam. Wakati Bunge la Tanzania likipitisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2020/21, wafanyabiashara wanaotangaza bidhaa kwenye magari watapata ahueni baada ada ya tozo za matangazo hayo kupunguzwa kwa asilimia 60. 

Bajeti hiyo ya Sh34.88 trilioni imepita baada ya wabunge 304 kupiga kura za ndiyo huku wabunge 63 wakipiga kura za hapana. Wabunge 13 hawakuwepo bungeni Jumatatu (Juni 15, 2020).

Bajeti hiyo itaanza kutekelezwa mwaka mpya wa fedha unaoanza Julai 1, 2020.

Katika mwaka ujao, Serikali pamoja na mambo mengine imesema itafanya marekebisho ya Kanuni za Ada ya Mabango na Matangazo (Local Government Finance (fees for Billboards, Posters and Hoarding) Order 2019), ili kupunguza kiwango cha tozo ya matangazo kwenye magari ya wazalishaji wa bidhaa yanayotumika kusafirisha bidhaa hizo toka viwandani kwenda kwa wasambazaji.

Marekebisho hayo ambayo yatafanyika katika mwaka wa fedha wa 2020/21 yatapunguza tozo kutoka kiwango cha sasa cha Sh10,000 hadi Sh4,000. 

Hiyo ni sawa na punguzo la asilimia 60 ya kiwango cha sasa.

“Lengo la mabadiliko haya ni kukidhi maombi ya wazalishaji dhidi ya tozo hii iliyosababisha wazalishaji wa bidhaa kuondoa matangazo kwenye magari hayo hivyo kupunguza mapato ya Serikali kutoka kwenye chanzo hicho,” amesema Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango katika hotuba ya bajeti ya 2020/21.


Soma zaidi:


Licha ya kuwa Serikali inataka kuongeza hamasa ya watu kutangaza bidhaa kwenye magari hayo, mabadiliko hayo yatapunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh1.25 bilioni.

Huenda hatua hiyo ya Serikali itasaidia wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo ikizingatiwa kuwa baadhi yao waliacha kutumia matangazo hayo kuepuka tozo hiyo. 

Februari 2019, Mkurugenzi Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Richard Kayombo alisema ni kawaida kwa magari yanayokuwa na matangazo kulipa tozo kwa sababu yanatazamwa na watu wengi yanapozunguka katika maeneo mbalimbali. 

“Siyo kodi mpya na si kitu cha ajabu, magari haya yanastahili kulipiwa, kwa mfano bango lipo katika gari linazunguka nchi nzima linaonwa na watu wengi zaidi kuliko bango lililowekwa sehemu moja,” alinukuliwa Kayombo na vyombo vya habari. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV

Sakata bei ya mafuta kupanda latua BoT, Naibu Gavana atoa ufafanuzi

Sakata bei ya mafuta kupanda latua BoT, Naibu Gavana atoa ufafanuzi

Nukta TV

BoT yabakiza Riba ya Benki Kuu 5.75% kudhibiti mfumuko wa bei

BoT yabakiza Riba ya Benki Kuu 5.75% kudhibiti mfumuko wa bei

Nukta TV