BoT yazipiga faini ya Sh1.8 bilioni benki tano Tanzania
- Benki hizo ni Equity, I&M, UBL, Habib African na African Corporation.
- Zimekiuka kanuni ya kuzuia utakatishaji fedha kwa kushindwa kuhakiki taarifa za utambulishjo wa wateja wao na kuwasilisha taarifa ya miamala yenye mashaka.
- Pia zimetakiwa kufanya tathmini ya ubora wa mifumo ya ndani ya kibenki ili kukinga mapaungufu hayo kujirudia tena.
Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezitoza faini ya Sh1.88 bilioni benki tano za biashara ikiwemo benki ya Equity kwa kukiuka kanuni ya kuzuia utakatishaji fedha kwa kushindwa kuhakiki taarifa za utambulisho wa wateja wao na kuwasilisha taarifa ya miamala yenye mashaka.
Taarifa iliyotolewa na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni African Banking Corporation ambayo imetozwa Sh145 milioni, Equity Bank (Sh580 milioni) na I&M (Sh655 milioni). Nyingine ni benki ya UBL (Sh325 milioni) na Habib African (Sh175 milioni).
“Benki Kuu ya Tanzania imezitoza faini benki tano za biashara kwa kukiuka kanuni namba 17, 22 na 28 za Kanuni za Kuzuia Utakatishwaji wa Fedha Haramu za mwaka 2012 kwa kushindwa kuhakiki taarifa za utambulisho wa wateja na kushindwa kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka katika Kitengo cha Kuzuia Fedha Haramu (FIU),” inasomeka sehemu ya taarifa ilitolewa kwa umma leo (Septemba 23, 2019).
Soma zaidi:
- BOT: Marufuku kurusha hovyo noti
- BOT yashusha tena riba kwa benki za biashara Tanzania
- NMB yaingiza sokoni huduma tatu za kidijitali kwa mpigo
Pamoja na faini hizo, BoT imezitaka benki hizo kupitia upyaPamoja na faini hizo, BoT imezitaka benki hizo kupitia upya taarifa za wateja wao na kuhakikisha kwamba zinakidhi matakwa ya kisheria na kanuni zilizopo za uhakiki wa utambulisho wa wateja (KYC) ndani ya kipindi cha miezi mitatu toka tarehe faini zilipotozwa.
“Kufanya tathmini ya ubora wa mifumo ya ndani ya kibenki na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa mifumo hiyo ipo madhubuti kwa lengo la kukinga mapungufu hayo hayarudii tena; na
“Kuwachukulia hatua stahiki za kinidhamu wafanyakazi wote waliohusika kufanikisha ufunguaji wa akaunti za amana kinyume na kanuni za kumtambua mteja (KYC),” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
BoT ambayo ni mlezi wa benki zote Tanzania imezikumbusha benki na taasisi za fedha kuhakikisha kuwa zinafuata sheria na kanuni zilizopo nyakati zote.
Hatua hiyo ya BoT imekuja ikiwa zimepita wiki 10 tangia ilipoitoza faini ya Sh1 bilioni benki ya DTB kwa kushindwa kuwa na Kituo cha Data (Data Center) nchini Tanzania licha ya kuthibitisha kuanzisha kituo cha pili cha data (Secondary Data Center).
Latest