BoT yazindua EMS kuimarisha ushindani na uwazi kwenye soko la dola Tanzania

June 9, 2026 4:57 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mfumo unaotajariwa kupunguza ucheleweshaji wa miamala na tofauti za viwango vya ubadilishaji kati ya taasisi mbalimbali za fedha.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua mfumo wa kielektroniki wa kuoanisha miamala (EMS) katika soko la jumla la fedha za kigeni, hatua inayotarajiwa kuongeza uwazi, ushindani na ufanisi katika biashara ya fedha za kigeni nchini.

Mfumo huo, uliozinduliwa Juni 8, 2026, utawawezesha mabenki ya biashara pamoja na wauzaji wakubwa wa bidhaa nje ya nchi watakaoidhinishwa na BoT kuwasilisha, kuoanisha na kufanya miamala ya fedha za kigeni kwa njia ya kielektroniki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Gavana wa BoT anayesimamia Sera za Uchumi na Fedha, Dk. Yamungu Kayandabila, amesema mfumo huo utaongeza uwazi na ufanisi katika upatikanaji wa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni.

“Tunategemea kuongezeka kwa ukwasi, kuimarisha ushindani na kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa soko,” amesema Dk Kayandabila.

Ni mfumo unaotajariwa kupunguza ucheleweshaji wa miamala na tofauti za viwango vya ubadilishaji kati ya taasisi mbalimbali za fedha. Picha | BoT

Aidha, ameongeza kuwa mfumo huo utaimarisha uwezo wa Benki Kuu katika kufuatilia shughuli za soko na kusaidia kuhakikisha kuwa soko la fedha za kigeni linaendelea kufanya kazi kwa utulivu, ufanisi na kwa kuzingatia viwango bora vya kimataifa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, washiriki wa EMS watafanya biashara kwa mfumo wa kutotambulika (anonymous trading), ambapo oda za ununuzi na uuzaji zitaoanishwa moja kwa moja kwa kuzingatia bei na muda wa kuwasilishwa kwa oda husika (price-time priority).

Suluhu viwango vya ubadilishaji fedha

Kwa miaka ya karibuni, soko la fedha za kigeni nchini limekuwa likikabiliwa na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, huku wafanyabiashara na waagizaji wa bidhaa wakilalamikia ucheleweshaji wa miamala na tofauti za viwango vya ubadilishaji kati ya taasisi mbalimbali za fedha.

Huenda kupitia mfumo huu mpya mahsusi kwa utekelezaji wa miamala ya papo kwa papo (spot transactions) kati ya Shilingi ya Tanzania na Dola ya Marekani, ukaleta upatikanaji wa viwango vya ubadilishaji vinavyoakisi hali halisi ya soko.

Endapo mfumo huo utaongeza ukwasi, uwazi na ushindani kama inavyotarajiwa, athari zake zinaweza kuonekana si tu katika sekta ya benki, bali pia kwa wafanyabiashara, wawekezaji na hatimaye kwa mwananchi anayeguswa na mabadiliko ya thamani ya shilingi na gharama za bidhaa zinazoagizwa kutoka nje. Picha | BoT

Hii ni kwa sababu kupitia EMS, BoT itaweza kuhamisha soko kutoka mfumo unaotegemea mawasiliano ya moja kwa moja kati ya washiriki kwenda mfumo wa kidigitali unaotoa fursa sawa kwa wote wanaoshiriki jambo linaloweza kupunguza mianya ya upendeleo katika utoaji wa bei na kuongeza ushindani miongoni mwa mabenki.

Endapo mfumo huo utaongeza ukwasi, uwazi na ushindani kama inavyotarajiwa, athari zake zinaweza kuonekana si tu katika sekta ya benki, bali pia kwa wafanyabiashara, wawekezaji na hatimaye kwa mwananchi anayeguswa na mabadiliko ya thamani ya shilingi na gharama za bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV