BoT yafungua soko la dhamana za Serikali kwa wawekezaji wa kigeni

August 10, 2026 2:31 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwekezaji yeyote asiye mkazi anaweza kushiriki katika dhamana za Serikali za muda mfupi na muda mrefu zinazotolewa na Serikali ya Tanzania.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefungua soko la dhamana za Serikali kwa kuwaruhusu wawekezaji wa kigeni kushiriki katika uwekezaji wa dhamana hizo, hatua inayoweza kuongeza mtaji wa kigeni na kuimarisha ukwasi katika soko la mitaji nchini. 

Kwa mujibu wa BoT, mabadiliko hayo yamefanyika kupitia Kanuni za Fedha za Kigeni (Marekebisho) za Mwaka 2026, ambazo zimetungwa chini ya Sheria ya Fedha za Kigeni, Sura ya 271.

Kabla ya marekebisho hayo, ushiriki wa wawekezaji wa kigeni katika soko la dhamana za Serikali ulikuwa ukihusisha wawekezaji kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Watanzania wanaoishi nje ya nchi pekee.

Hivyo kwa marekebisho yaliyofanyika mwekezaji yeyote asiye mkazi anaweza kushiriki katika dhamana za Serikali za muda mfupi na muda mrefu zinazotolewa na Serikali ya Tanzania, akizingatia masharti yaliyowekwa na sheria na taratibu za BoT.

BoT imesema hatua hiyo inalenga kupanua wigo wa ushiriki katika soko la dhamana za Serikali na ni sehemu ya juhudi za kuendeleza masoko ya fedha nchini pamoja na kuifanya Tanzania kuwa kituo chenye mvuto wa uwekezaji.

“Hatua hii inalenga kupanua wigo wa ushiriki katika soko la dhamana za Serikali na ni sehemu ya jitihada za Benki Kuu za kuendeleza masoko ya fedha nchini na kuitangaza Tanzania kama kitovu chenye fursa za uwekezaji,” imeeleza taarifa ya BoT.

Akizungumzia mabadiliko hayo, mtaalamu wa fedha na uchumi kutoka Dar es Salaam, Paul Chengula, amesema hatua hiyo ina manufaa kwa Tanzania kwa sababu inaweza kuongeza mahitaji ya Shilingi endapo wawekezaji wa kigeni wataingia nchini kuwekeza katika dhamana za Serikali.

“Wawekezaji watakapokuja kuwekeza katika dhamana za Serikali, watahitaji fedha yetu, hivyo demand ya shilingi itaongezeka. Hii inaweza kusaidia kuimarisha thamani ya fedha yetu na hatimaye kuimarisha uchumi,” amesema Chengula.

Kwa mujibu wa Chengula, kuongezeka kwa wawekezaji katika soko la dhamana kunaweza pia kuongeza mzunguko wa fedha na shughuli za kiuchumi, huku Serikali ikipata wigo mpana wa kupata fedha kupitia soko la mitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
10 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
10 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
10 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
EXCLUSIVE: Fahamu ukweli kuhusu kunyonyesha na kumbemenda mtoto | PART 1

EXCLUSIVE: Fahamu ukweli kuhusu kunyonyesha na kumbemenda mtoto | PART 1

Nukta TV

Rais Samia aipa miezi 5 Tume ya Uchunguzi jinai Oktoba 29

Rais Samia aipa miezi 5 Tume ya Uchunguzi jinai Oktoba 29

Nukta TV

Rais Samia ataja sababu kushirikisha wajumbe kutoka nje, Tume ya Uchunguzi makosa ya jinai Oktoba 29

Rais Samia ataja sababu kushirikisha wajumbe kutoka nje, Tume ya Uchunguzi makosa ya jinai Oktoba 29

Nukta TV