Bidhaa za vyakula zachangia kushuka mfumuko wa bei Tanzania

November 9, 2023 12:04 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Washuka kwa asilimia 1 kutoka asilimia 3.3 iliyorekodiwa mwaka unaoishia Septemba 2023 mpaka asilimia 3.2 mwaka unaoishia Oktoba mwaka huu.
  • Kushuka huko kunaashiria ahueni kiduchu katika bei za bidhaa za chakula nchini.

Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania kwa mwaka unaoishia Oktoba 2023 imepungua kwa asilimia moja ikichangiwa na kupungua kwa bei za bidhaa za  vyakula ikiwemo ngano, mchele na nyama.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa mfumuko wa bei nchini iliyotolewa Novemba 8, 2023 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kasi ya mfumuko wa bei imepungua kutoka asilimia 3.3 iliyorekodiwa mwaka ulioishia  Septemba 2023 hadi asilimia 3.2 kwa mwaka unaoishia mwezi Oktoba mwaka huu.

“Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2023…” imeeleza taarifa ya NBS.

Samaki wakavu wameshuka kwa moja kutoka asilimia 6.9 hadi asilimia 6.7.Picha|K14

Kwa mujibu wa NBS, bidhaa hizo za chakula zilizochangia kushuka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na ngano kutoka asilimia 3.1 hadi asilimia 2.4, mchele (kutoka asilimia 7.6 hadi asilimia 4.4), samaki wabichi (kutoka asilimia 8.0 hadi asilimia 7.1) na dagaa wakavu kutoka asilimia 13.5 hadi asilimia 11.0

Nyingine ni samaki wakavu kutoka asilimia 6.9 hadi asilimia 6.7, matunda (kutoka asilimia 10.4 hadi asilimia 6.1), mihogo mibichi (kutoka asilimia 7.4 hadi asilimia 7.1), magimbi (kutoka asilimia 13.6 hadi asilimia 11.3), maharage (kutoka asilimia 16.3 hadi asilimia 10.3), choroko kavu (kutoka asilimia 3.0 hadi asilimia 1.1) na njegere kavu kutoka asilimia 8.6 hadi asilimia 8.4.

Kushuka kwa bei ya bidhaa hizo kunaashiria unafuu kiduchu katika upatikanaji wa bidhaa kulinganisha na miezi mitatu iliyopita mabapo kiwango cha mfumuko wa bei kiling’ang’ania asilimia 3.3.

Aidha, NBS imeeleza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Oktoba, 2023 nao umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 5.6 uliyorekodiwa mwaka ulioishia Septemba, 2023. 

Kwa upande wa mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba, 2023 umeongezeka kidogo na kufikia asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.4 iliyorekodiwa mwaka ulioishia Oktoba, 2023.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV