Bei ya mahindi yapaa Morogoro

January 17, 2022 2:02 pm · Wilson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya mahindi yapaa kwa asilimia 56 Mkoa wa Morogoro
  • Tabasamu zaidi kwa wakulima na wafanya biashara na vilio kwa walaji.

Dar es salaam. Bei ya jumla ya mahindi katika mkoa wa Morogoro imepada katika kipindi cha wiki moja,  jambo linalowapa kicheko wakulima na wafanyabiashara.

​Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Januari 14, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo mkoani humo linauzwa kwa Sh150,000 kutoka Sh66,604 kama ilivyorekodiwa wiki iliyopita Januari 10, 2022. 

Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 56 (Sh66,604) ndani ya kipindi cha wiki moja.

Kupanda kwa bei ya zao hilo katika Mkoa wa Morogoro huenda kukabadili mwelekeo wa kibiashara katika masoko mbalimbali hususani yaliyo jirani na Mkoa huo na kuwaingizia faida zaidi wakulima na wafanyabiashara.

Bei inayotumika leo mkoani Morogoro ndiyo ya juu zaidi Tanzania Bara huku bei ya chini ikirekodiwa mkoani Ruvuma kwa Sh50,000. 


Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV