Kufa kufaana: Bei ya mahindi yazidi kupaa tanzania

August 8, 2022 5:17 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Gunia la kilo 100 liliuzwa Sh78,163 Juni mwaka huu.
  • Bei hiyo imeongezeka kwa asilimia 82.3 ndani ya mwaka mmoja.
  • Serikali yasema hatafunga mipaka.

Dar es Salaam. Huenda Watanzania wakaendelea kutoboa mifuko yao zaidi baada ya bei ya mahindi kupanda kwa asilimia 82.3 hadi kufikia Sh78,163 mwaka unaoshia Juni 2022.

Mahindi ni sehemu ya mazao makuu ya chakula yanayotumiwa kwa wingi. Mazao mengine ni maharage, mtama, uwele na viazi.

Ripoti ya Mapitio ya Uchumi ya Julai 2022 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa bei ya jumla ya gunia la kilo 100 la mahindi kwa mwaka ulioishia Juni 2021 ilikuwa inauzwa kwa Sh Sh42,757 lakini imepanda hadi Sh78,163 Juni mwaka huu. 

Ni kawaida katika kama hiki ambacho wakulima wanakuwa wametoka kuvuna bei za mazao kushuka lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti.

BOT katika ripoti hiyo imeeleza kuwa hali hiyo imesababishwa na mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa ambapo msimu wa kilimo ulipata mvua chache na hivyo kupunguza kiwango cha uzalishaji.

“Kuongezeka kwa bei kunahusishwa na kuongezeka uhitaji wa chakula nchi za jirani na kupungua kwa mavuno kulikosababishwa na uchache wa mvua,” imeeleza BoT.

Kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kunawaumiza walaji kwa sababu wanalazimika kutoboa zaidi mifuko yao zaidi ili kupata zao hilo la chakula, wakati wakulima wananeemeka na bei hiyo.

Hata wakati bei ya mahindi ikipaa kwa asilimia 82.3 zaidi ya ile ya mwaka 2021, bei hiyo imekuwa ikipanda mfululizo tangu Machi mwaka 2022.

Machi bei ya jumla ya  mahindi ilikuwa Sh60,996 ikapanda mwezi uliofuata na kufikia Sh62,542 kabla haijapanda zaidi Mei na kuuzwa Sh69,771 na Juni ikapanda hadi Sh78,163.

Bei hiyo iliyotumika Juni 2022, ndiyo bei ya juu zaidi kuwahi kufikiwa mwaka mmoja uliopita unaoishia Juni.


soma zaidi


Hatufungi nchi, chakula kipo cha kutosha

Mbali na kupanda kwa bei ya bidhaa za vyakula, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliyekuwa kwenye Maonyesho ya Wakulima ya Nane Nane mkoani Mbeya wiki hii alisema uzalishaji wa mazao ya chakula haujashuka, kiasi cha kushindwa kuhimili  mahitaji ya nchi hivyo mipaka haitafungwa kuwezesha mazao kuuzwa nje ya nchi.

“Tumefungua mipaka na hatutafunga mipaka…mahali ambapo tutaona bei imepanda sana tutapeleka  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) waende wakauze kwa bei ya nafuu,” alisema Waziri Bashe.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV