Ajira 1,056 zanukia kwa watunza kumbukumbu Tanzania

October 31, 2024 10:29 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ajira hizo ni zile zitakazotolewa kwa mwaka 2024/25
  • Waziri Simbachawene asema idadi hiyo ya ajira ni kubwa kuliko miaka mingine.

Arusha. Serikali ya Tanzania imesema inatarajia kuajiri watunza kumbukumbu 1,056  katika mwaka wa fedha 2024/25 ili kukabiliana na uhaba wa watumishi hao.

Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene amesema idadi hiyo ya watumishi watakaoajiriwa kwa mwaka huu ni kubwa kulinganisha miaka iliyopita.

Simbachawene ameyasema hayo wakati  akizungumza katika mkutano wa 12 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbumbukumbu na Nyaraka Tanzania (Trampa) uliofanyika leo Oktoba 30,2024 mkoani Dodoma.

“Bajeti ya mwaka huu tumepata vibali vya kuajiri watumishi 1,056 idadi hii ni kubwa kulinganisha na miaka mingi nyuma, ni hatua inayohitaji kupongezwa sana tumpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuijali kada hii na kutupa vibali vingi kuliko miaka mingi iliyopita,” amesema Simbachawene.

Mbali na idadi hiyo, Waziri Simbachawene amesema kuwa wataajiri watunza kumbukumbu wasaidizi 1,041, huku nafasi 15 pekee zikiwalenga watunza kumbukumbu wenye elimu ya ngazi ya shahada.

Kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la wanaohitimu kada hiyo kwa ngazi ya shahada Simbachawene amesema atafanya mazungumzo na katibu mkuu wa wizara yake kuona uwezekano wa kuongeza nafasi hizo kwa wahitimu ngazi hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, aliyekuwa mgeni rasmi wa mkutano huo amezitaja faida za kada hiyo nchini kuwa ni pamoja na kuisaidia Serikali kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Kumbukumbu na nyaraka zinasaidia serikali kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na nyenzo muhimu ambazo zinamsaidia Mkaguzi  na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua na kuthibitisha uhalali wa matumizi ya fedha za umma,”amesema Abdulla.

Faida nyigine kwa mujibu wa kiongozi huyo ni kuboresha vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato kwa kuwa kupitia  taarifa zilizohifadhiwa tunafahamu maeneo ya uwekezaji yakiwemo ya utalii na hatimaye kukuza pato la Taifa na kuchangia uimarishaji wa miradi ya maendeleo.

Kutokana na umuhimu huo amewataka watunza kumbukumbu hao kusimamia maadili ina miiko ya taaluma kwa kuwa ndiyo msingi mkuu wa kulinda kada zote nchini.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV