Dola ya Marekani yaongezeka kwa Sh10 NMB, yabaki tulivu CRDB
- Sarafu nyingine ikiwemo Pauni ya Uingereza na Euro zimeonyesha mabadiliko kidogo.
Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeongezeka kwa Sh10 katika Benki ya NMB, wakati Benki ya CRDB imeendelea kubakiza viwango vyake bila mabadiliko.Â
kwa mujibu wa Benki ya NMB, Dola ya Marekani (USD) leo inanunuliwa kwa Sh2,595 kuiuza kwa Sh2,675 sawa na iliyokuwa ikitumika jana.
Kwa upande wa CRDB, dola imeendelea kununuliwa kwa Sh2,605 na kuuzwa kwa Sh2,685, viwango vilivyodumu kwa juma zima.
Hii inamaanisha kuwa wanunuaji wa sarafu hiyo kupitia benki ya NMB watanunua dola kwa bei nafuu zaidi.
