Shilingi yaendelea kuimarika dhidi ya Euro na Pauni, Dola yabaki tulivu

July 22, 2026 8:58 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ishara kwamba mahitaji na upatikanaji wa dola umeendelea kuwa katika uwiano mzuri. 

Dar es Salaam. Soko la fedha za kigeni nchini limeendelea kubaki tulivu Julai 22, 2026 huku Dola ya Marekani ikiendelea kubaki katika viwango vilevile vya jana, wakati Euro na Pauni ya Uingereza zikiendelea kushuka kidogo dhidi ya shilingi ya Tanzania.

Takwimu za viwango vya fedha zinazotolewa na benki za NMB na CRDB zinaonyesha kuwa Dola ya marekani imeendelea kununuwa kwa Sh2,595 na kuuzwa kwa Sh2,675 katika benki zote mbili ishara kwamba mahitaji na upatikanaji wa dola umeendelea kuwa katika uwiano mzuri. 

Kwa upande wa Euro, shilingi imeonyesha kuimarika kidogo. CRDB imeshusha kiwango cha kununua Euro kutoka Sh2,857.70 hadi Sh2,856.43 na kiwango cha kuuza kutoka Sh3,157.70 hadi Sh3,156.43. 

NMB nayo imepunguza kiwango cha kununua kutoka Sh2,871 hadi Sh2,868 huku kiwango cha kuuza kikishuka kutoka Sh3,143 hadi Sh3,140.

Mwenendo kama huo umeonekana kwa Pauni ya Uingereza. CRDB imepunguza bei ya kununua Pauni kwa zaidi ya Sh17, kutoka Sh3,392.69 hadi Sh3,375.42, huku bei ya kuuza ikishuka kutoka Sh3,692.69 hadi Sh3,675.42. 

NMB pia imepunguza kiwango cha kununua kutoka Sh3,355 hadi Sh3,334 na kiwango cha kuuza kutoka Sh3,700 hadi Sh3,679.

Kwa upande wa sarafu za kikanda Sarafu ya Kenya (KSH) na Shilingi ya Uganda (UGX) vimeendelea kubaki bila mabadiliko katika benki zote mbili, jambo linaloashiria utulivu wa sarafu hizo katika kipindi cha siku moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
22 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
22 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
22 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kozi nzuri za kusoma chuo

Kozi nzuri za kusoma chuo

Nukta TV

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Nukta TV

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Nukta TV