Yuani yaendelea kuimarika taratibu dhidi ya Shilingi ya Tanzania

July 16, 2026 8:35 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko hilo ni dogo ukilinganisha na mabadiliko yanayojitokeza kwenye sarafu kama Euro na Pauni ya Uingereza.

Dar es Salaam. Wakati sarafu kuu za kimataifa kama Dola ya Marekani, Euro na Pauni ya Uingereza zikiendelea kutawala soko la fedha za kigeni, takwimu za viwango vya ubadilishaji fedha vya leo Julai 16, 2026 vinaonesha kuwa Yuani ya Uchina (CNY) imeendelea kuimarika taratibu dhidi ya Shilingi ya Tanzania.

Takwimu za Benki za CRDB na NMB zinaonesha kuwa mwenendo wa Yuani umeendelea kupanda kwa kiwango kidogo tangu mwanzoni mwa Julai,1 mwaka huu hali inayoashiria kuongezeka kwa thamani yake katika soko la fedha za ndani.

Kwa mujibu wa viwango vya Benki ya CRDB leo Yuani imenunuliwa kwa Sh366.01 na kuuzwa kwa Sh411.01, ikilinganishwa na Julai 14, ambapo ilinunuliwa kwa Sh365.22 na kuuzwa kwa Sh410.22 ikiwa ni ongezeko la Sh0.79 katika viwango vyote vya kununua na kuuza ndani ya siku mbili.

Kwa upande wa Benki ya NMB, Yuani imenunuliwa kwa Sh381 na kuuzwa kwa Sh420, kutoka Sh380 na Sh419 zilizorekodiwa Julai 14 mwaka huu. Hivyo, benki hiyo pia imerekodi ongezeko la Sh1 kwa viwango vya kununua na kuuza, likiashiria mwelekeo unaofanana na ule wa CRDB.

Ingawa ongezeko hilo ni dogo ukilinganisha na mabadiliko yanayojitokeza kwenye sarafu kama Euro na Pauni ya Uingereza, hali hii inamanisha kuwa Yuani imeendelea kupata nguvu taratibu katika soko la ubadilishaji fedha nchini.

Maana yake kwa wafanyabiashara

Kuimarika kwa Yuani kunamaanisha kuwa waagizaji wa bidhaa kutoka China watahitaji kutumia Shilingi nyingi zaidi kupata kiwango kilekile cha fedha za Kichina. 

Hali hiyo inaweza kuongeza gharama za uagizaji wa bidhaa mbalimbali, hususan mashine, vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme, nguo na bidhaa nyingine zinazotoka China.

Kwa upande mwingine, wafanyabiashara na kampuni zinazopokea malipo kwa Yuani wanaweza kunufaika kwa kupata Shilingi nyingi zaidi wanapobadilisha fedha hizo katika benki za ndani.

Kwa ujumla, pamoja na mabadiliko hayo ya Yuani, soko la fedha za kigeni nchini linaendelea kuonesha utulivu, huku ongezeko la thamani ya sarafu hiyo likiwa la taratibu na lenye kufuatiliwa kwa karibu na wafanyabiashara wanaofanya biashara na soko la China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV