FIFA kuuza kipande cha nyasi uwanja wa fainali Kombe la Dunia kwa Sh1 milioni

July 17, 2026 12:06 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vipande kutoka uwanja wa New York New Jersey nchini Marekani, kipande kikubwa zaidi kuuzwa Sh8 milioni.

Dar es Salaam. Mbio za fainali za Kombe la Dunia zinaendelea kuchanja mbuga huku mashabiki wa nyota wa soka Lionel Messi wakiendelea kutembea kifua mbele mara baada ya timu wa taifa ya Argentina kufanikiwa kumng’oa mwingereza kwa bao moja kwa mbili kwenye hatua ya nusu fainali.

Hata hivyo kivumbi na jasho kinatarajiwa kuonekana siku ya Jumapili Julai 19, 2026 ambapo kidume wa mashindano haya makubwa zaidi ya michezo duniani atakwenda kuonekana baada ya dakika 90 za mtanange kati ya Argentina na Hispania kutamatika katika dimba la New York New Jersey nchini Marekani.

Mchezo huu wa fainali hauendi tu kuwa mchezo wa kawaida bali kwa kila timu inakwenda kuandika historia mpya itakaponyakua taji hilo lenye thamani zaidi kuliko mataji yote katika ulimwengu wa soka.

Kwa Argentina iwapo atashinda anakwenda kuweka historia ya kuchukua kombe hilo mara mbili mfululizo tangu atwae taji hilo mwaka 2022 pale nchini Qatar kitu ambacho ni nadra sana kufanyika katika historia ya soka.

Kadhalika kwa Hispania iwapo atashinda atakwenda kumaliza ukame wa miaka 16 tangu kutwaa taji hilo mwaka 2010 pale Afrika Kusini chini ya kizazi cha kina Xavi na Iniesta.

Lakini kwa mwaka huu kuna jambo la kushangaza kidogo kwani Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) halijataka historia ya mtanange huo kubakia katika picha na video tu na badala yake imetangaza kuuza vipande vya nyasi za uwanja utakapochezeka mchezo huo ambao kuushudia live itakulazimu kununua tiketi kwa zaidi ya Sh15 milioni kwa daraja la kawaida.

Kwa mujibu wa FIFA vipande hivyo vya nyasi vinakwenda kuuzwa kama bidhaa maalum ya ukumbusho, huku bei zikianzia dola 450 za Marekani, ambayo kibongo bongo ni zaidi ya Sh1 milioni kwa kipande kimoja.

Kwa mashabiki wanaotaka kumbukumbu ya kiwango cha juu zaidi, kuna vifurushi vinavyofikia hadi dola 3,000 ambayo ni takriban Sh8 milioni. 

Ikiwa FIFA itafanikiwa kuuza idadi yote ya vipande maalum vilivyowekwa, taasisi hiyo inatarajia kuingiza kiasi cha Dola za Marekani milioni 11 zaidi ya Sh29 bilioni.

Je, upo tayari kununua kipande cha nyasi kwa Sh1 milioni?,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV