Ng’andi: Chakula cha asili chenye virutubishi vingi

August 9, 2022 3:26 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Mahitaji ya chakula hiki ni ndizi maharage,mafuta ya kupikia, kitunguu, karoti, hoho na magadi.

Wachaga wana vyakula vingi vya kiutamaduni ambavyo huliwa kwenye  matukio mbalimbali. Kuna mtori, ngararimo,  kitawa, ng’andi, kiburu na vingine vingi kutegemea na ukanda mpishi anapotokea.

Nimemtembelea Jojina Kinabo (mama Diana) anayeishi jijini Dar es Salaam  ambaye amenifundisha jinsi ya kupika ng’andi za kichaga, nimeona nikuletee na wewe ujuzi huu  uweze kubadilisha menyu lakini pia uweze kuonja ladha hii ya kipekee ya watu wa kaskazini.

Ng’andi ni jina la kichaga lenye kumaanisha chakula cha ndizi na maharage kilichosongwa. Mahitaji ya chakula hiki ni ndizi maharage,mafuta ya kupikia, kitunguu, karoti, hoho na magadi.

Chakula hiki kina mahitaji machache na ni rahisi kukipika, tukaribie jikoni tupike ng’andi.

Maandalizi

Menya ndizi, zioshe na uzikate kwa saizi ndogo ndogo, chambua maharage na uyaoshe tayari kwa ajili ya kuyabandika.

 Mimi nimeyaloweka maharage yangu kwa masaa 12, ili iwe rahisi kuyapika kwenye gesi.

Mama Diana aliiniambia enzi zao walikuwa wanapikia kuni tena kwenye chungu ilichukua saa nne mpaka matano kuivisha chakula hiki.

“Heri yenu sasa hivi kuna gesi mnapika kwa haraka, tofauti na enzi zetu” anasema mama Diana.

Baada ya kuchemsha maharage, yakishaiva weka ndizi kwa juu na maji kidogo mpaka ziive.

Ongeza na magadi au “mbaala” kama unavyoitwa kwa kichaga

Zikiiva anza kuzisonga taratibu bila kugusa maharage ya chini, zikisagika zichanganye na maharage kwa kuzikoroga kwa pamoja na maji kiasi. 

Kwenye sufuria ya pembeni kaanga kitunguu, karoti na hoho kisha uweke mchanganyiko wako wa ndizi na maharage.

Funika kidogo zichemke, ukihakikisha maji yamekauka na kubaki na mchuzi mzito hapo ng’andi zako zitakuwa tayari.

Mbali na chakula hiki kuliwa na watu wa rika zote, chakula hiki kina protini nyingi yenye kujenga mwili.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV