Aina tatu za mapishi ya mtori wa ndizi

March 9, 2023 3:24 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Chakula hiki kinafaa kwa watoto wadogo, wagonjwa na wazazi waliotoka kujifungua.
  • Ni rahiisi kuandaa unaweza kutumia kipekecho, blenda au mwiko.

Mtori  ni moja kati ya chakula maarufu kinachotumika zaidi wakati wa asubuhi kwa watu wazima au watoto.

Chakula hiki kimejizolea umaarufu mwingi sehemu mbalimbali nchini, huku kikisindikizwa na vitafunwa mbalimbali kama chapati na maandazi.

Kwa watoto wadogo, wagonjwa na wazazi waliotoka kujifungua chakula  hiki kimekuwa sehemu ya mlo wao wa siku unaowapatia nguvu na ladha ya kipekee.

Kuna aina mbalimbali za mapishi ya chakula hiki. Mapishi ya mtori kwa kutumia kipekecho (kifaa cha asili kinacho tumika kusaga chakula), blenda au kusaga kawaida na mwiko.

Leo tutajifunza aina hizo tatu rahisi ambazo unaweza kupika nyumbani na ukaachana na habari ya kununua mgahawani au hotelini.

Tuingie jikoni sasa

Maandalizi ya awali ya pishi hili ni pamoja na kuandaa nyama kwa kuikata kata na kuisaga, kitunguu swaumu, tangawizi na jiko la kisha ubandike na uache iive.

Wakati unasubiri nyama kuiva andaa ndizi kwa kuzimenya na kuziosha, kitunguu maji, karoti, hoho, maji ya ndimu na nyanya kama utapendelea.

Baada ya hapo chemsha ndizi zako mpaka ziive  tayari kwa kuandaa mtori.

Mtori wa kusaga kwa kutumia kipekecho

Mara baada ya nyama na ndizi kuiva anza kwa kuweka ndizi kwenye bakuli safi au sufuria kisha uziponde ndizi kwa kipekecho taratibu na kuondoa mabonge yote.

Baada ya hapo anza kusaga kwa kupekecha taratibu huku unaongeza supu ya nyama taratibu mpaka ndizi zako zilainike kabisa.

Rudia hatua hiyo mpaka uridhishwe na ulaini wa mtori wako kisha rudisha jikoni ongeza supu iliyobaki,mafuta ya kupikia  chumvi, kitunguu, karoti hoho na uache uive kwa dakika tano na mtori wako utakuwa tayari.

Kipekecho ni kifaa cha asili kinachotumika kusaga vyakula mbalimbali kama mtori na mlenda.Picha|Ika Malle/YouTube

Mtori  wa kusaga na blenda

Aina hii ya mapishi inafaa sana kwa watu wenye haraka, unachotakiwa kufanya ni kuweka ndizi zako zilizoiva kwenye  blenda, ongeza supu na usage mpaka zilainike.

Hakikisha ndizi zako zimepoa ndipo usage pia uweke kidogo kidogo ikiwa una ndizi nyingi.

Baada ya hapo mimina mchanganyiko wako kwenye sufuria ongeza supu iliyobaki,mafuta ya kupikia kiasi, chumvi, kitunguu, karoti hoho na uache uive kwa dakika tano na mtori wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Unaweza pia kuweka kitunguu na viiungo vingine ulivyonavyo kabla ya kusaga na kuchanganya mtori wako.Picha|Ivie’s Cuisine.

Mtori wa kusaga na mwiko

Hapa pia hakuna mambo mengi ni kuponda tu ndizi kwenye sufuria kwa kutumia mwiko mpaka mabonge yote yaishe.

Rudia tena kuponda huku ukiongeza supu taratibu mpaka iwe laini kabisa kwa kiwango unachotaka.

Ukiridhishwa na ulaini huo basi rudisha jikoni pika kwa moto mdogo kwa dakika 5 ongeza supu iliyobaki, mafuta ya kupikia kiasi na viungo vingine vyote kisha unaweza kutenga.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV