Fahamu namna ya kuandaa chakula cha ‘loshoroo’

September 2, 2022 9:33 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Chakula hiki huifadhiwa kwenye kibuyu cha asili.
  • Huliwa  na watu wa rika zote.
  • Mahitaji yake ni pamoja na mahindi yaliyokobolewa na na maziwa ya mgando.

Ni chakula maarufu kaskazini mwa Tanzania. Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya mgando na mahindi yaliyokobolewa na hufadhiwa kwenye kibuyu cha asili.

Loshoroo ni chakula cha asili cha kabila la Wamasai na Wameru wanaopatikana kaskazini mwa Tanzania.

Huliwa na watu wa rika zote. Hata watoto na wazee wasiokuwa na meno wanaweza kula kutokana na uwepo wa maziwa.

Kiasili chakula hiki huifadhiwa kwenye kibuyu ili kisiharibike kwa haraka. Kikihifadhiwa vizuri kinaweza kukaa hata wiki moja bila kuharibika. Kinapoendelea kukaa kwenye kibuyu huwa kichachu ndipo utamu wake ulipo.

Maandalizi

Washa jiko bandika sufuria yenye maji yakishapata moto weka mahindi.

Ongeza maji kila yanapokaribia kuisha ili mahindi yako yaive. Yanaweza kuchukua muda wa saa mbili au tatu.

Mahindi yakishaiva yaipue ili yapoe, yakishapoa weka maziwa ya mgando na uyakoroge, yaache kama dakika tano yajichanganye vizuri hapo yatakuwa tayari.

Baada ya chakula chetu kuwa tayari, unaweza kuhifadhi kwenye kibuyu. Wakati wa kula unaweza kuweka kwenye kikombe au bakuli.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV