Mambo ya kuzingatia wakati unapika urojo

July 23, 2024 3:53 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakikisha hauachi jikoni kwa muda mrefu mpaka ukaungua.
  • Usiweke maji mengi ukawa mwepesi kupitiliza.

Urojo ni mchanganyiko wa vyakula mbalimbali pamoja na uji uji wake katika bakuli moja.

Asili ya urojo ni kutoka nchini India lakini umejipatia umaurufu Tanzania pia. Leo nakupa maujanja ya kupika chakula hiki ambacho unaweza kutumia nyumbani na biashara.  

Urojo wako ukiiva unaweza kuula na viazi mviringo vya kuchemsha, mayai ya kuchemsha, bagia, chachandu ya nazi, chipsi za muhogo, mishikaki, kachori, katlesi na pilipili. 

Tuingie jikoni

Hatua ya kwanza weka unga kwenye bakuli kisha weka maji nusu lita pamoja na binzari. Baada  ya hapo koroga hadi uhakikishe mabonge yote yameisha kisha mimina maji yaliyo baki kwenye sufuria na weka chumvi kiasi  na uache yachemke  kwa dakika 20. 

Hatua inayofuata ni kumimina uji wenye binzari kwenye maji ya moto taratibu huku ukikoroga mpaka uchanganyike. Acha uchemke kidogo kwa dakika 5 kisha mimina ndimu yako na ukoroge kidogo na hapo unaweza onja chumvi na ndimu kama zipo sawa  ndio utoe jikoni.

Kata viazi mviringo ulivyovichemsha vipande vidogo vidogo. Menya mayai kata vipande vinne, chukua bakuli na kijiko weka vipande vya viazi ulivyovikata.

Baada ya hapo malizia kuweka kachori, bagia, mishkaki, chipsi za muhogo na katlesi, kisha mimina urojo kiasi upendacho, weka chachandu ya nazi na pilipili.

Kufikia hapo urojo utakuwa tayari kwa ajili ya kutumiwa mezani. 

Unataka tukufundishe pishi gani katika makala inayofuata? Dondosha maoni yako kupitia WhatsApp namba 0750 0881 888. 

Angalizo:

  • Kama urojo ukiwa na chumvi nyingi ongeza maji. 
  • Hakikisha hauachi jikoni kwa muda mrefu mpaka ukaungua.
  • Usiweke maji mengi ukawa mwepesi kupitiliza.
Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV