Yaliyojiri bajeti ya Wizara ya Maendeleo na Vijana ikisomwa kwa mara ya kwanza

April 20, 2026 4:40 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Vipaumble, changamoto na mikakati ya kuwainua vijana ni miongoni mwa yalijadiliwa.

 Dar es Salaam. Bajeti ya Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana imesomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Dodoma leo Aprili 20, 2026 tangu kuanzishwa rasmi kwa wizara hiyo na Rais Samia Suluhu Novemba 17 mwaka jana.

Akiwasilisha bajeti hiyo leo Aprili 20, 2026 bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Joel Nanauka ameliomba Bunge liidhinishe Sh35.9 bilioni kwa mwaka wa fedha 2026/27 ili kutekeleza shughuli mbalimbali za wizara hiyo.

Awali masuala ya vijana yalikuwa yakishuguhulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu chini ya Waziri Ridhiwani Kikwete

Kwa mujibu wa Rais Samia lengo la kuanzisha wizara hiyo ni kuhakikisha vijana wanapata jukwaa la kusikika na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi.

Pamoja na kuanzishwa kwa wizara hiyo Rais Samia aliahidi  kuanzisha kitengo cha washauri wa vijana ndani ya ofisi ya Rais.

Akizungumza leo Aprili 20, 2026 bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Joel Nanauka, ameeleza kuwa kati ya bajeti hiyo inayosubiri kuidhinishwa na Bunge Sh30.1 bilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Katika kiasi hicho cha matumizi hayo ya kawaida, Sh1.22 bilioni ni kwa ajili ya mishahara, huku Sh28.8 bilioni zikiwa kwa matumizi mengineyo (OC). 

Kwa upande mwingine Sh5.85 bilioni zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo Sh5 bilioni ni fedha za ndani na Sh853.03 milioni ni fedha za nje.

Aidha, Nanauka amesisitiza ukubwa na umuhimu wa kundi la vijana nchini, akibainisha kuwa zaidi ya vijana milioni 20, sawa na asilimia 34.4 ya Watanzania, wanachangia zaidi ya asilimia 55 ya nguvu kazi ya taifa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA)

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA)

Nukta TV

Yaliyojiri Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana ikisomwa kwa mara ya kwanza

Yaliyojiri Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana ikisomwa kwa mara ya kwanza

Nukta TV

Maendeleo ya Vijana yaomba kuidhinishiwa Sh35.9 bilioni bajeti 2026/27

Maendeleo ya Vijana yaomba kuidhinishiwa Sh35.9 bilioni bajeti 2026/27

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.