Gharama, elimu ya kidigitali vikwazo vya ukuaji wa ‘Fintech’ Tanzania

March 26, 2026 4:51 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Zaidi ya watumiaji milioni 300 wamejisajili kutumia huduma za ujumuisha wa kifedha kwa njia nya kidigitali.

Dar es Salaam. Licha ya teknolojia ya kifedha (‘Fintech’) kuendelea kukua nchini Tanzania wadau wa sekta ya fedha wamebainisha vikwazo vinavyoweza kurudisha nyuma jitihada za ukuaji wa teknolojia hizo.

Fintech ni jumla ya teknolojia zote zinazotumika katika sekta ya kifedha, ikijumuisha benki, mifumo ya malipo na biashara za kielektroniki, ambazo hurahisisha upatikanaji wa huduma na usalama wa kifedha kwa watumiaji.

Kennedy Komba Mkurugenzi wa Ujumuishaji na Upanuzi wa Huduma za Kifedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) aliyekuwa akizungumza leo Machi 26,2026 amesema Fintech inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu ya digitali.

“Vikwazo bado vipo, kama vile gharama kubwa ya intaneti, ukosefu wa elimu ya kidijitali na uhitaji wa bidhaa zinazozingatia mahitaji ya mteja..,” amesema Komba katika Jukwaa la Uwekezaji Afrika Mashariki (EAIF 2026) jijini Dar es Salaam.

Jukwaa hilo limewakutanisha wawekezaji, wafanyabiashara wadogo na wa kati, wabunifu wa teknolojia, watunga sera na taasisi za fedha kwa lengo la kujadili njia za kukuza ubunifu, kuvutia mitaji na kuleta mabadiliko yenye tija. Picha| Infocus

Komba anafafanua kuwa changamoto nyingine inayoikabili sekta hiyo ni mgawanyiko wa kidijitali jambo ambalo linafanya maeneo ya mijini kukua kwa kasi kidijitali huku vijijini wakiendelea kukabiliana na vikwazo vinavyohusiana na kuunganishwa kwa mtandao na elimu ya kidigitali. 

“Safari ya kuelekea uchumi wa kidigitali unaojumuisha kila mtu ni mbio za masafa marefu, si mbio za muda mfupi. Inahitaji ushirikiano endelevu, uundaji wa sera madhubuti, na ahadi ya kumweka mlaji katika kitovu cha kila kitu tunachofanya,” amesema Komba.

Pamoja na uwepo wa changamoto hizo Komba amebainisha kuwa mwaka 2025 zaidi ya watumiaji milioni 300 walijisajili kutumia huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali huku upatikanaji wa huduma hiyo nchini ukifikia asilimia 95.

Mkurugenzi wa Kukuza Ujumuishaji wa Kifedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Kennedy Komba akiongea kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu. Picha| Infocus.

Huenda ongezeko hilo la matumizi ya Fintech yalichangiwa zaidi na kuongezeka kwa watumiaji wa intaneti nchini kutoka milioni 40 mwaka 2024 hadi miliioni 58.1 kama ilivyoainishwa katika ripoti ya robo ya nne ya mwaka 2025 inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ufumbuzi watolewa

Ili kutatua changamoto hizo, Komba ameeleza kuwa BoT imeanzisha mfumo unaoruhusu kampuni changa za Fintech kufanya majaribio ya uvumbuzi wao chini ya uangalizi kabla ya kuingia sokoni rasmi.

Vilevile, inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Ujumuishi wa Kifedha (National Financial Inclusion Framework) unaolenga kutoa kipaumbele kwa masuluhisho ya kidijitali yanayomlenga mteja wa mwisho.

Mwenyekiti wa Tanzania Fintech Association, Cynthia Ponera awali akizungumza na wadau mbalimbali katika jukwaa hilo. Picha| Infocus.

Awali akizungumza katika jukwaa hilo Mwenyekiti wa ‘Fintech’ Cynthia Ponera, amesema upatikanaji wa huduma za mikopo na akiba ni msingi wa maendeleo jumuishi hasa wakati ambao mafanikio ya sekta hiyo yanategemea mshikamano wa ubunifu, uthabiti pamoja na uwepo wa mifumo rafiki ya kisheria.

/
No matches found for this filter
23 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV