Hizi ndizo Passport 5 zenye nguvu zaidi Duniani

July 22, 2026 2:58 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na Passort ya Singapore, Japan, Finland, Denmark na New Zealand.

Dar es Salaam. Umewahi kujikuta unatumia muda mrefu katika ofisi ya balozi ya nchi fulani ili kupata viza ?

Basi fahamu kuwa baadhi ya watu duniani, usumbufu huo wanausikia TikTok. Pasipoti zao zinatosha kuingia katika nchi mbalimbali. 

Pasipoti ni hati ya kusafiria ambayo humwezesha raia wa taifa moja kuingia taifa lingine kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kazi, biashara, utalii au hata kula bata tu.

Licha ya kumiliki pasipoti, nchi mbalimbali humuhitaji msafiri kupata viza katika ubalozi wa nchi husika ili apate kibali cha kuingia katika nchi hiyo. Zipo nchi duniani ambazo pasipoti zao zina nguvu ambapo raia wake wanaweza kusafiri katika nchi mbalimbali bila kuhitaji viza. 

Kila mwaka, nguvu ya pasipoti hupimwa kwa kuangalia ni nchi ngapi mmiliki wake anaweza kuingia bila kuhitaji viza, au kwa kupata viza anapowasili (Visa on Arrival). 

Kadiri idadi hiyo inavyoongezeka, ndivyo pasipoti hiyo inavyokuwa na nguvu zaidi.

Kwa mujibu wa Henley Passport Index, shirika la kimataifa ambalo hupanga passport za dunia kwa kutumia takwimu rasmi za Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA), zipo passport ambazo zinawapa wamiliki wake uhuru wa kutembelea karibu kila kona ya dunia bila viza. 

Hizi ndio pasipoti 5 zennye nguvu zaidi duniani hadi kufikia 2026 kwa mujibu wa Henley Passport Index.

5. New Zealand

Ukizungumza nchi yenye ushawishi mkubwa duniani, New Zealand haiwezi kukosekana.

Mbali na mandhari yake ya kuvutia na uchumi imara, passport ya nchi hiyo ina thamani kubwa duniani. Mmiliki wa passport ya New Zealand anaweza kusafiri katika nchi zaidi ya 185 bila kuhitaji viza ya awali.

Hii inamaanisha kuwa mmliki huyu amebakiza mataifa 10 tu ambayo ndio pekee anahitaji Viza ili kuingia. Diniani kuna nchi 195. 

Nguvu hiyo imejengwa na miaka mingi ya uhusiano mzuri wa kidiplomasia, viwango vya juu vya usalama pamoja na imani ambayo nchi zimeweka kwa raia wa nchi hiyo.

4. Denmark

Denmark ni mojawapo ya nchi ambazo zimejijengea sifa ya utawala bora, uchumi imara na maisha yenye ubora wa hali ya juu.

Nje ya sifa hizo, Passport yake ni silaha ya kusafiria duniani.

Raia wa Denmark wanaweza kuingia katika zaidi ya nchi 188 bila viza ya awali, jambo linaloifanya kuwa moja ya passport zinazotamaniwa zaidi duniani.

Kwa kuwa ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na eneo la Schengen, wananchi wake wanafurahia uhuru mkubwa wa kusafiri, kufanya kazi na kuishi katika nchi za Ulaya bila vikwazo.

3. Finland

Huenda wengi wanaifahamu kama taifa ambalo wananchi wake ndio wenye furaha zaidi duniani 

Lakini zaidi ya furaha hiyo, Pasipoti ya nchi hiyo ina nguvu ya kipekee.

Raia wa Finland wanaweza kutembelea zaidi ya nchi 189 bila viza ya awali au kwa kupata viza wanapowasili.

Hii inamaanisha mmiliki wa Passport hii anaweza kutembelea dunia yote isipokuwa nchi 6 tu. 

Nguvu ya passport ya Finland inachangiwa na diplomasia ya kimataifa, kiwango cha chini cha migogoro ya kisiasa na uaminifu mkubwa wa hati zake za kusafiria.

2. Japan

Kwa zaidi ya muongo mmoja, Japan imeendelea kuwa miongoni mwa mataifa yanayobadilishana nafasi ya kwanza katika orodha ya passport zenye nguvu zaidi duniani.

Leo, passport yake ni tiketi inayoweza kumfikisha mmiliki wake katika mataifa 190 duniani bila viza ya awali au kwa kupata viza anapowasili.

Nguvu ya Passport ya Japan ni matokeo ya uchumi imara, teknolojia ya hali ya juu, utulivu wa kisiasa na uhusiano wa kidiplomasia uliotengenezwa kwa miongo mingi.

Kwa Wajapani, kusafiri duniani mara nyingi ni jambo rahisi kuliko ilivyo kwa mamilioni ya watu kutoka mataifa mengine ambao hulazimika kupitia mchakato mrefu wa kuomba viza.

1. Singapore

Na juu ya wote, ipo Singapore

Kwa miaka ya hivi karibuni, passport ya Singapore imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani kwa wamiliki kuingia bila viza.

Mmiliki wa passport ya Singapore anaweza kusafiri katika nchi 193 bila kuomba viza kabla ya safari hii ni sawa na asilimia 97 ya nchi zote 195 duniani bila vikwazo vyovyote.

Nguvu hiyo si bahati mbaya. Ni matokeo ya sera madhubuti za kidiplomasia, uchumi wenye ushindani mkubwa na uhusiano mzuri wa kimataifa uliodumu kwa miongo kadhaa.

Ni muhimu kufahamu kuwa nguvu ya passport haimaanishi utajiri wa mtu binafsi bali ni kiwango cha uhuru wa kusafiri ambacho taifa lake limejenga kupitia diplomasia, usalama na uaminifu wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
22 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
22 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kozi nzuri za kusoma chuo

Kozi nzuri za kusoma chuo

Nukta TV

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Nukta TV

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Nukta TV