Nini hutokea kichwani unapokunywa pombe?
- Kuzima kimya kimya kwa mawasiliano ya Ubongo
- kuanza kuona kilevi kama kipaumbele kuliko raha za kawaida.
Dar es Salaam: Kila siku, mamilioni ya watu duniani pote hunywa pombe kwa ajili ya kusherehekea matukio mbalimbali, huku wengine wakiitumia kujifurahisha na kuupa mwili pole baada ya mihangaiko ya siku nzima.
Licha ya kinywaji hicho kuonekana kuwa sehemu ya maisha wataalamu wa afya wamekuwa wakipiga vita unywaji wa pombe hususan ule wa kupitiliza kutokana na madhara yake kiafya na kijamii.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) takriban watu milioni 400, sawa na asilimia 7 ya watu wote duniani wenye umri wa miaka 15 na kuendelea, waliishi na matatizo ya matumizi ya pombe.
Kati yao, watu milioni 209 (asilimia 3.7) waliangukia kwenye uraibu wa kinywaji hicho.
Safari ya madhara ya pombe huanza punde tu unapomeza fundo la kwanza kinywani na kuteremeka hadi kwenye tumbo na baadae kwenye utumbo mdogo ambapo hufyonzwa kuingia kwenye damu na baadae kwenye viungo kama figo, Ini na ubongo.
Mara nyingi madhara yanayojitokeza katika viungo vingine hutokea taratibu kulinganisha na madhara yanayotokea katika ubongo ambayo huanza kuonekana ndani ya dakika chache tu.
Yafuatayo ni mambo muhimu yanayotokea katika ubongo wa binadamu dakika kadhaa anapokunywa fundo chache za pombe.
Wataalam wanasemaje?
Wataalamu wengi duniani wamekuwa wakipiga vita unywaji wa pombe kutokana na madhara yake kiafya na kijamii. Unywaji wa pombe umeendelea kuathiri watu wengi kupitia matukio mbalimbali, ikiwemo ajali, matatizo ya afya ya akili pamoja na matumizi ya madawa mengine yatokanayo na uraibu wa pombe.
Akizungumza na Nukta Habari, Dk. Saboya James kutokea India amesema kuwa vichocheo vilivyomo kwenye pombe husababisha madhara makubwa zaidi pale mtumiaji anapoitumia kupita kiasi, hali inayoharibu mfumo wa fahamu na kumfanya kushindwa kufanya maamuzi sahihi katika nyanja mbalimbali za maisha.
“Mtu anapotumia pombe kwa wingi, madhara yake huwa makubwa zaidi. Ubongo huathirika kwa kiwango kikubwa, hali inayomfanya mtu kupoteza uwezo wa kufikiri kwa umakini, kufanya maamuzi yasiyo sahihi, kuingia kwenye uraibu wa pombe na hatimaye kuathirika kwa mfumo wake wa maisha ya kila siku, ikiwemo hali ya kiuchumi,” amesema Dk James.
Ameongeza kuwa, licha ya kuwepo kwa uwezekano wa mtu mwenye uraibu wa pombe kuacha kabisa unywaji huo na kurejea katika hali ya kawaida, bado yapo madhara ya kimwili ambayo huweza kubaki maisha yote. Madhara hayo ni pamoja na ulemavu wa kudumu kama kupooza (paralysis), hali ambayo huwa ni vigumu kurejea katika hali ya kawaida.
Latest