HESLB yaongeza muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo

September 1, 2025 4:42 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa lengo la kuwapa fursa wanafunzi ambao hawakuweza kuwasilisha maombi yao kwa wakati waweze kuwasilisha.

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imeongeza muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kutoka  Agosti 31 hadi Septemba 14, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bodi muda huo umeongezwa ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawakuwasilisha maombi yao kwa wakati kuwasilisha.

Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo ya wanafunzi kwa njia ya mtandao kuanzia Juni 15, 2025, hadi na ilipangwa Agosti 31 kuwa tamati.

Kwa mujibu wa HESLB hadi Agosti 31, jumla ya maombi 157,309 yamepokelewa, ikiwa ongezeko la asilimia 5 ikilinganishwa na maombi 150,530 yaliyokuwa yamepokelewa mwaka jana. 

“Aidha, maombi 960 ya ‘Samia Scholarship’ yamepokelewa, ikilinganishwa na 742 mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 29,” imeeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, HESLB imesisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2025, hivyo waombaji wanatakiwa kukamilisha maombi yao ndani ya muda huo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV