Lissu kuendelea kusota rumande kwa zaidi ya siku 90, shauri lake likisogezwa mbele 

July 15, 2025 6:28 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Upande wa Jamhuri waomba shauri liahirishwe kuipa muda Mahakama Kuu kutolea majibu maombi yao.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu ataendelea kusota mahabusu kwa zaidi ya siku 90 sasa, mara baada ya shauri la uhaini namba 8607/2025 linalomkabili kuahirishwa mpaka Julai 30.

Shauri hilo limeahirishwa kufuatia upande wa Jamhuri kuomba kesi iahirishwe baada ya wao kupeleka maombi Mahakama Kuu ya kutaka mashahidi katika kesi hiyo watoe ushahidi kwa kificho kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kulinda usalama wao.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Franco Kiswaga aliridhia ombi hilo na kueleza kuwa sababu ya kuahirishwa kesi iliyotolewa na upande wa Jamhuri ina mashiko.

Tundu Lissu ataendelea kusota mahabusu kwa zaidi ya siku 90 sasa, mara baada ya shauri la uhaini namba 8607/2025 linalomkabili kuahirishwa mpaka Julai 30. Picha | DW

Maombi ya upande wa Jamhuri ambayo yaliwasilishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai yamepingwa na mshtakiwa Lissu kwa kudai kuwa hakuna sababu ya msingi kwa upande wa Jamhuri kupewa ahirisho jingine. 

“Walitakiwa wapeleke kwanza hiyo taarifa Mahakama Kuu, haizuii hayo maombi walioomba. Kwanini hawajapeleka taarifa Mahakama Kuu?, kwa sababu wanacheza na Mahakama yako, kwa sababu unawaruhusu,” amehoji mshtakiwa Lissu mahakamani hapo.

Mbali na pingamizi la ahirisho la shauri linalomkabili, Lissu aliwasilisha ombi jingine la kuiomba Mahakama kutumia Mamlaka ya Msingi ya Kuzaliwa nayo (Inherent Power) kumfutia mashataka na kumuacha huru.

Hata hivyo, Hakimu Kiswaga ameeleza kuwa, mahakama hiyo haiwezi kutumia Mamlaka ya Msingi ya Kuzaliwa nayo kwa sababu shauri hilo lipo katika hatua ya kupelekwa Mahakama Kuu (Committing stage) na sio hatua ya usikilizwaji (Listening stage).

Lissu aliwasilisha ombi la kuiomba Mahakama kutumia Mamlaka ya Msingi ya Kuzaliwa nayo (Inherent Power) kumfutia mashataka na kumuacha huru. Picha | IPP Media

Mbali na maamuzi yaliyotolewa, Mahakama imeutaka upande wa Jamhuri kutotumia nafasi iliyotolewa na Mahakama kuchelewesha uendeshwaji wa shauri hilo na kuwataka kushughulikia maombi waliyopeleka Mahakama Kuu kwa uharaka.

Lissu anatimiza siku 97 tangu alipokamatwa na Jeshi la Polisi Aprili 9, 2025 alipokuwa katika mkutano wa kisiasa wa chama chake mkoani Ruvuma.

Kwa mara ya kwanza Lissu alifikishwa mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Aprili 10, 2025 ambapo shauri linalomkabili litaendelea kusikilizwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV