Viwango vya kubadili fedha za kigeni leo Desemba 13, 2024

December 13, 2024 10:06 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Ndani ya wiki hii thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika kila siku dhidi ya dola ya Marekani iliyokuwa ikinunuliwa kwa Sh2,500.61 na kuuzwa Sh2,525.62 Disemba 10, 2024. Kwa muda wa siku nne hadi kufikia leo Disemba 13 thamani ya dola kununuliwa imepungua kwa Sh205.91 na kuuzwa Sh2,294.7 wakati ya kuuza ikipungua kwa Sh208.02 hali inayotoa ahueni kwa wafanyabiashara wanaotumia dola kuagiza bidhaa.

Kutoka jana Disemba 12 thamani ya kununua dola imepungua kwa Sh64.45 huku ya kuuza ikipungua kwa Sh65.15 kwa mujibu wa viwango vya Benki Kuu.

Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika pia dhidi ya sarafu za Euro kutoka Disemba 10 kwa Sh240.5 sambamba na sarafu ya China (CYN) kwa Sh28.48 kwa bei za kununua wakati Euro ikipungua kwa Sh243.17 sambamba na CYN kupungua Sh28.71.

kwa kipindi cha wiki moja bei ya dhahabu pia imeendelea kushuka kila siku, kutoka jumanne Disemba 10 bei ya kukua imepungua kwa Sh365,493 sambamba na ya kuuza kwa Sh367,444. Kutoka jana bei ya kununua imeshuka kwa Sh159,943 na ya kuuza kwa Sh162,611.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks