Wanafunzi 70,990 wapatiwa mkopo wa elimu ya juu Tanzania

October 21, 2024 11:41 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  •  Kati ya wanafunzi hao wanaume 40,164 na wanawake ni 30,825.
  • Mkopo huo umegharimu Sh 233.3 bilioni.

Arusha. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Heslb) imesema wanafunzi 70,990 wa mwaka wa kwanza wamepatiwa mkopo wenye thamani ya Sh 233.3 bilioni kwa ajili ya muhula mpya wa masomo 2024/25.

Taarifa ya Dk Bill Kiwia, Mkurugenzi Mtendaji wa Heslb iliyotolewa Oktoba 21 inafafanua kuwa idadi hiyo imefikiwa baada ya kutangazwa kwa wanafunzi wengine 19,345 waliopangiwa mkopo katika awamu ya tatu.

“Heslb imetangaza awamu ya tatu (Batch Three) yenye wanafunzi 19,345 wa shahada ya awali waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Sh 59.49 bilioni kwa mwaka wa masomo 2024/2025,” imesema taarifa ya Dk Kiwia.

 Kati ya wanafunzi hao waliopata mkopo katika awamu zote tatu kwa msimu wa masomo 2024/25 wanaume 40,164 sawa na asilimia 56.5 na wanawake ni 30,825 sawa na asilimia 43.4.

Aidha, Heslb pia imesema imetoa mikopo kwa wanafunzi wapya wa stashahada 425 wakiwemo wa  mwaka wa kwanza 378 na wanaoendelea na masomo 47.

Mikopo hiyo kwa ngazi ya stashahada ina thamani ya  Sh1.1 bilioni huku wanafunzi wengine 599 wa mwaka wa kwanza wakinufaika na ruzuku ya ‘Samia Scholarship’ yenye thamani ya Sh 3 bilioni.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV