Serikali yaongeza kikokotoo pensheni ya wastaafu Tanzania

June 13, 2024 1:27 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Sasa wastaafu watalipwa malipo yao ya mkupuo ya asilimia 40  kutoka asilimia 33 inayotumika sasa.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema itaongeza malipo ya mkupuo ya kikokotoo cha pensheni ya wastaafu kutoka asilimia 33 iliopo sasa hadi asilimia 40 lengo likiwa ni kuimarisha maslahi ya watumishi hao.

Mabadiliko haya yanakuja ikiwa ni siku 42 tu tangu Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aahidi maboresho katika suala hilo huku akisistiza kuwa maboresho hayo yatatokana na tathmini ya kina ya kisayansi ya watakwimu bima. Dk Mpango aliyasema hayo Mei 1, 2024 alipokuwa akihutubia katika siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika kitaifa jijini Arusha. 

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba aliyekuwa akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25 bungeni Dodoma leo Juni 13, 2024 amesema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa watumishi hao.

“Serikali yetu sikivu inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan, imesikia kilio hicho na imekifanyia kazi kwa maslahi mapana ya wastaafu wetu na wanaotarajiwa kustaafu… ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliopo sasa hadi asilimia 40,” amesema Dk Mwigulu.


Soma zaidi: Mustakabali wa kikokotoo cha mafao bado kizungumkuti Tanzania


Waziri huyo amesema ongezeko hilo ni kwa watumishi waliokuwa wakilipwa asilimia 50 hapo awali ambao walishushwa hadi asilimia 33, ikiwa ni theluthi tu ya penshen yao.

Kwa upande wa watumishi waliokuwa wakipokea malipo ya mkupuo ya asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33, Dk Nchemba amesema sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka huu wa fedha unaoanza Julai mosi.

Huenda mabadiliko haya yakafuta machozi ya watumishi pamoja na wabunge wao waliokuwa wakipaza sauti bungeni wakitaka Serikali kuongeza kikokotoo hicho na ikiwezekana wastaafu wapewe zaidi ya asilimia 50 ya mafao yao ili kujiendeleza kiuchumi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV