Ukopeshaji sekta binafsi watarajiwa kuongezeka mara mbili Tanzania 2021

September 28, 2020 1:08 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • BoT yasema kiwango cha ukopeshaji kinatarajiwa kuongeza hadi asilimia 11.6 ifikapo Juni 2021.
  • Kiwango cha ukopeshaji kwa sekta hiyo kwa miezi miwili ya Juni na Julai, 2020 kilikuwa asilimia 5.5.
  • Riba ya mikopo inayotolewa na benki za biashara nayo yapungua. 

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mwenendo wa ukopeshaji sekta binafsi upo imara ukienda sanjari na matarajio ya kufikia kiwango cha asilimia 11.6 ifikapo Juni 2021 jambo litakalowapa fursa wafanyabiashara kupata mitaji ya kuendesha biashara zao.

Matarajio hayo ya BoT ifikapo Juni 2021 ni mara mbili ya kiwango cha ukopeshaji kwa sekta binafsi kilichorekodiwa Juni 2020 cha asilimia 5.5. 

Ripoti ya Tathmini ya Uchumi ya mwezi Agosti 2020 (Economic Monthly Review) iliyotolewa na BoT hivi karibuni inaeleza kuwa mikopo kwa sekta binafsi kwa mwaka ulioishia Julai 2020 ilikuwa asilimia 5.5 sawa kabisa ilivyokuwa mwaka ulioishia Juni mwaka huu. 

Kuongezeka kwa mikopo kwa sekta hiyo kunatoa fursa kwa biashara na watu binafsi kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli za za kibiashara ili kujipatia faida na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. 

BoT imesema kiwango hicho cha mikopo kwa sekta binafsi kwa miezi ya Juni na Julai mwaka huu kinalingana na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Soma zaidi: 


Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza kuwa sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuelekezwa kwa watu binafsi ambao walipata wastani wa takriban theluthi moja au asilimia 32.4 ya mikopo yote ikifuatiwa na shughuli za biashara (asilimia 16.8) na uzalishaji hasa viwandani kwa asilimia 10.9.

Mikopo inayoelekezwa katika shughuli zote kubwa za uchumi imeendelea kuongezeka, isipokuwa kwa shughuli za madini, biashara, kilimo, hoteli na migahawa katika kipindi hicho cha mwaka ulioishia Julai 2020. 

“Kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kulichangiwa na usimamizi thabiti wa sera ya fedha na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kuboresha mazingira ya biashara,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo inayopatikana pia katika tovuti ya BoT.

Hata wakati mikopo kwa sekta binafsi ikitarajiwa kuongezeka zaidi, riba inayotozwa na benki za biashara nayo imeshuka kutokana na usimamizi thabiti wa sera za fedha unaofanywa na Serikali jambo ambalo ni kiasharia kizuri kwa ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi,

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, riba iliyotozwa kwenye mikopo iliyotolewa na benki ilikuwa wastani wa asilimia 16.55 mwezi Julai 2020 ikishuka kutoka wastani wa asilimia 16.87 katika kipindi kama hicho 2019.

Kupungua kwa riba za benki hupunguza maumivu ya urejeshaji mikopo kwa wananchi wengi zaidi wakiwemo wakulima kunufaika na huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi hizo za fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV