Majaliwa atoa maagizo mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Tanzania

February 9, 2021 1:14 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ameitaka mifuko inayotoa dhamana kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kutathmini shughuli na huduma zake ili kubaini mafanikio na changamoto.
  • Amesema Serikali inataka mikopo itolewe kwa masharti nafuu zaidi na riba ndogo kuliko ilivyo sasa.
  • Jambo hilo litakuwa ni ahueni kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kwani litarahisisha upatikanaji wa mikopo.

Dar es Salaam.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza mifuko na programu zote za uwezeshaji wananchi kiuchumi zifanye tathmini ya shughuli na huduma zake ili kubaini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji uboreshaji hususan eneo la masharti ya utoaji mikopo kwa wajasiriamali.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo (Februari 9, 2021) wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya nne ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi yanayoendelea katika viwanja vya Shiekh Amri Abied jijini Arusha. 

Amesema Serikali inataka mikopo itolewe kwa masharti nafuu zaidi na riba ndogo kuliko ilivyo sasa. Na mipango maalumu itakayoandaliwa na mifuko hiyo iwasilishwe Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na baadaye taarifa za utekelezaji zitolewe katika kipindi cha kila robo mwaka.

“Jiepusheni na vitendo vya rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Pia, watendaji wa mifuko na programu za uwezeshaji pamoja na taasisi za fedha hakikisheni mnatoa huduma bila urasimu wala ubaguzi wa aina yoyote. 

“Nasisitiza wananchi wanapofika kwenye ofisi zenu wapokelewe kwa staha, wasikilizwe na kupatiwa huduma stahiki kwa wepesi.” amesema Majiliwa.


Soma zaidi:


Waziri huyo pia ametoa wito kwa vyombo mbalimbali vya habari kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo ili viweze kufikisha ujumbe sahihi kuhusu fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mifuko na programu za uwezeshaji kwa wananchi wote nchini.

“Takwimu zinaonesha kwamba katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015/16 hadi 2019/20 mifuko na programu za uwezeshaji za Serikali zimefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh2.22 trilioni na hivyo, kunufaisha zaidi ya watu milioni 4.9 na taasisi 5,499,” amesema Majaliwa. 

Kwa mujibu wa Majaliwa, Halmashauri 185 Tanzania Bara zimefanikiwa kutoa Sh93.3 bilioni kupitia mifuko ya uwezeshaji wa makundi maalum ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu zinazosaidia upatikanji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi 32,553.  

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amesema baraza linaratibu mifuko na programu za uwezeshaji zipatazo 55, ambapo kati yake mifuko ni 48 na programu saba.

“Mifuko hii imeanzishwa kwa ajili ya kutatua changamoto zinazozuia wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, ambazo ni pamoja na ufinyu wa vyanzo vya akiba na mapato, kutokuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba, kuwepo kwa masharti magumu ya mikopo, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa dhamana na riba kubwa zinazotozwa na mabenki kwenye mikopo.” amesema Issa.

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

Nukta TV

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

Nukta TV