Umevuka miaka 40? Mafanikio bado yanakusubiri!

August 30, 2018 5:21 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Mafanikio hayaangalii umri bali ni mipango inayoambatana na bidii, uvumilivu kufikia malengo.
  • Wakati mwingine hali ngumu ya maisha inafikirisha zaidi kuelekea mafanikio ya kweli.

Dar es Salaam. Huenda wewe ni miongoni mwa watu waliovuka miaka 40 na unajisikia vibaya kwasababu hujapata mafanikio uliyokusudia? Usijali hauko peke yako. Wapo watu mashuhuri ambao walikuwa na maisha magumu katika ujana wao lakini baadaye walifanya mambo makubwa yaliyobadilisha maisha yao baada ya kuvuka umri wa miaka 40. 

Ipo mifano mingi ya watu kutoka nyanja mbalimbali ambao wanathibitisha kuwa sio lazima ufanye kila kitu au ufanikiwe ukiwa na umri wa miaka 30. Hawa ni baadhi ya watu waliokamilisha ndoto zao walipovuka miaka 40: 

Colonel Sanders

Anafahamika zaidi kama Colonel Harland Sanders ni mwanzilishi wa migahawa ya KFC duniani. Licha ya kustaafu akiwa “fukara wa kutupwa” katika umri wa miaka 65, lakini hadi wakati anafariki (1980) akiwa na umri wa miaka 90 alikuwa katika orodha ya mabilionea wakubwa nchini Marekani.

Kwa sasa migahawa ya KFC imeenea katika nchi 123 duniani, Tanzania ikiwemo. NIi mgahawa wa pili kwa ukubwa duniani baada ya mgahawa ya McDonald’s wa nchini Marekani.

Mwaka 2013 migahawa ya KFC ulifanya mauzo ya Dola za Marekani 23 bilioni. Maana yake ni kwamba mauzo ya KFC kwa mwaka mmoja ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka miwili.

     Sanders hakukata tamaa ya kuyatafuta mafanikio mpaka alipofikia ndoto za kumiliki mgahawa mkubwa duniani. Picha| Bingedaily

Kumbuka muasisi huyo alikuwa fukara hadi uzee wake wa miaka 65 na akadhani ameshindwa maisha. Akajaribu kujiua. Lakini baada ya kutafakari akaona bado ana nafasi ya kujaribu tena. Akajaribu japo katika umri wa uzee, na hatimaye Mungu akamfanikisha. Akawa Bilionea mkubwa sana nchini Marekani.


Vera Wang

Ni Mwanamitindo mashuhuri duniani mwenye asili ya China lakini kabla ya kufikisha miaka 40 alikuwa Mwandishi wa habari na mwanamichezo wa michezo ya barafu. Mafanikio na jina lake lilianza kusikika alipoingia kwenye tasnia ya mitindo ya mavazi akiwa na umri wa miaka 40. Na sasa anatambulika kama mwanamke bora wa kusanifu nguo zinazotumiwa na watu maarufu wakiwemo wasanii na wanasiasa.

Vera Wang; mafanikio yalimfuata alipoamua kubadilisha fani aliyoizoea awali. Picha| femalefirst.co.uk

Henry Ford

Alizaliwa mwaka 1863 huko Michigan Marekani na ndiye mwanzilishi wa Kampuni ya Magari ya Ford. Alianza kusikika baada ya kutengeneza gari aina ya Model T mwaka 1908 ambalo lilileta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri. 

Alitengeneza gari hilo akiwa na umri wa miaka 45 na mapaka leo anatambulika kuwa miongoni mwa matajiri waliokuwa na kipato kikubwa katika karne ya 19.

Henry Ford siku za uhai wake. Picha| ThoughtCo

Charles Dawn

Alikuwa mwanasayansi aliyebobea kwenye sayansi ya miamba, uumbaji na biolojia. Alizaliwa na kukulia nchini Uingereza lakini mwaka 1859 akiwa na miaka 50 alitoa nadharia yake ya binadamu wanatokana na sokwe ‘The Origin of Species’ ambapo alibadilisha kabisa mtazamo wa jamii kuhusu dhana ya uumbaji mpaka leo, watu wengi wanaamini binadamu ametokana na sokwe.

Nadharia za Dawn zilileta mabadiliko makubwa katika fikra za watu kuhusu uumbaji wa binadamu. Picha|elsoldelbajio.com.mx

Betty White

Huyu alizaliwa mwaka 1922 huko Marekani ni muigizaji wa filamu za vichekesho na amepata tuzo nyingi kutokana na umahiri wake wa kuigiza na kuvuta hisia za watu wengi nchini humo. Lakini kilichompa umaarufu ni kujiunga na kipindi cha runinga cha ‘The Mary Tyler Moore Show’  mwaka 1973 akiwa na umri wa miaka 51. Alijipatia mashabiki wengi na fedha nyingi kutokana na kipaji chake cha kuigiza.

Kipaji chake cha kuigiza filamu kilimtoa kimaisha. PIcha| yahoo.com

Wakati mwingine utakapokuwa unafikiria kwanini umefikisha miaka 40 lakini bado ni maskini, itakupasa ufikirie mara mbili kabla ya kukata tamaa na kuona maisha yamefika mwisho. Mafanikio hayaangalii umri bali ni mipango inayoambatana na bidii, uvumilivu kufikia malengo uliyojiwekea.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV