TMA yatahadharisha ujio wa mvua kubwa

September 26, 2018 9:53 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Mvua hiyo itakuwa katika mkoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
  • Mvua hizo zinaweza kusababisa mafuriko katika mitaa na foleni kali maeneo ya mjini. 

Dar es salaam. Ndani ya siku tatu zijazo huenda  hali ya Jiji la Dar es Salaam ikabadilika ghafla baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutahadharisha kutokea kwa mvua kubwa kuanzia Septemba 26 hadi Septemba 27, 2018.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TMA leo jioni (Septemba 25,2018) imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hiyo ni baadhi ya maeneo ya  mikoa ya Dar es salaam, Tanga na Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Utabiri huo kutoka TMA umewataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari kwa sababu mvua hizo.


Yanayokuhusu: Watanzania washauriwa kutumia taarifa za hali ya hewa kwenye mipango ya maendeleo 

                             Ujio mfumo wa taifa wa hali ya hewa kuchochea ujenzi wa viwanda nchini

                             Usafiri, biashara kuwa sehemu ya mwelekeo hali ya hewa Dar


TMA imeeleza madhara yanayoweza kutokana na mvuo hizo kwa wananchi na mali zao.

“Madhara yatakayotokana na mvua hiyo ni kutokea mafuriko katika mitaa na kusababisa msongamano wa magari na watu hivyo kuchelewasha usafirishaji hasa katika maeneo ya mjini,’’ imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Enable Notifications OK No thanks