Dk Abbas atoa maana ya “kuikosoa Serikali”

November 24, 2018 11:39 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Msemaji Mkuu wa serikali Dk Hassan Abbas amekanusha uvumi unaonezwa na baadhi ya watu kuwa “kuikosoa Serikali ni marufuku”wakati alipokuwa anazungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (TUDARCO). Picha| Rodgers Raphael.


  • Amesema changamoto iliyopo ni kushindwa kutofautisha kati ya kuikosoa na kuitukana Serikali kwani wengi wamekuwa wakitukana na kusema wanaikosoa.
  • Uhuru wa kutoa maoni umeelezwa vizuri katika Sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 ambayo imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wadau kuwa inaminya uhuru wa kujieleza.

Dar es Salaam. Msemaji Mkuu wa serikali Dk Hassan Abbas amewapinga vikali watu wanaosema “kuikosoa Serikali ni marufuku” kwasababu uhuru wa kutoa maoni umeelezwa vizuri katika Sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016.  

 Dk Abbas ametoa msimamo huo wakati akizungumza na wahadhili na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (TUDARCO) kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo nchini ambapo amesema mtu yeyote anaweza “kuikosoa Serikali”.

 “Watu wanasema uhuru hamna kwa sababu haiwezekani kuikosoa serikali, huo ni uzushi unaweza kuikosoa serikali,” amesema Dk Abbas.

Pamoja na kutoa ufafanuzi huo, Dk Abbas amesema wadau wa vyombo vya habari nchini wanapaswa kutofautisha kati ya kuikosoa na kuitukana Serikali kwani wengi wamekuwa wakitukana na kusema wanaikosoa.

Amesema Wanahabari wanapaswa kufahamu haki zao za msingi wakati akitimiza majukumu ya kikazi ikiwemo kukusanya, kuhariri na kuchapisha habari ili kutekeleza haki ya watu wengine ya kupata taarifa sahihi. 


Zinazohusiana: 


Akizungumzia utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, amewatoa hofu Wanahabari kwa kusema sheria hiyo itawezesha kuanzishwa Bodi ya urasimishaji wa wanahabari (Journalist accreditation Board) pamoja na Kamati ya malalamiko (complains committee) ambayo itasaidia kupunguza adha na kero za Wanahabari.

”Vyombo hivi vitakuwa mwamvuli kwa wadau wa sekta ya habari na waandishi wa habari kupeleka malalamiko yao,” amesema Dk Hassan

Katika maelezo yake amesema sheria hiyo imeweka wazi kwa mara ya kwanza tangu nchi kupokea uhuru mambo mbalimbali yenye manufaa kwa Wanahabari ikiwemo kutokuwahusisha wachapishaji endapo gazeti lolote litachapisha taarifa zisizo za ukweli.

Mwanafunzi wa chuo TUDARCO, Leyla Siraj amesema ufafanuzi wa utekelezaji wa sheria hiyo umemfungua macho kutokana na kuelewa maudhui yaliyopo ndani.  

“Watu walikua wakilalamika sana juu ya sheria mpya lakini kumbe wengi hulalamika kwa maneno ya kuambiwa na wenzao ambao huenda hata hawajaisoma sheria hiyo, pia niimefahamu uzuri wa sheria hii kwa upana Zaidi,” amesema Siraj.

Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 alianza kutumika baada ya Rais John Magufuli kuweka saini Novemba 16, 2016 ikiwa ni siku chache ilipopitishwa na Bunge siku ya Novemba 5, 2016 Jijini Dodoma.

Licha ya mambo mazuri yanayotajwa katika sheria hiyo, bado utekelezaji wake na sheria kama Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2016 ambazo zote zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kutoa maoni.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV