Taboa mbioni kuja na mfumo wa kukata tiketi za mabasi kielektroniki
- Unaratibiwa na Chama Cha Wamiliki wa Mabasi.
- Utawawezesha abiria kukata tiketi za mabasi popote walipo kwa simu na kompyuta.
- Tenda yatangazwa kwa wabunifu wa teknolojia kutengeneza mfumo huo.
Dar es Salaam. Huenda wasafari wanaokwenda katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania wasilazimike tena kwenda kwenye ofisi za mabasi kukata tiketi,baada ya Chama Cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) kutangaza tenda ya kwa ajili ya kutengeza mfumo wa ukataji tiketi wa kielektroniki.
Tenda hiyo iliyotangazwa Februari 11 ,2020 inawataka waombaji kutengeneza mfumo ambao utamfanya mtumiaji kukata tiketi akiwa popote na kumuwezesha kuona siti za gari analotaka kusafiria.
‘Mfumo huo lazima uwe na uwezo wa kutumika katika mifumo tofauti ili kumwezesha mtu kukata tiketi,mifumo hiyo ni pamoja na meseji (USSD), tovuti, POS devices (mashine za mauzo) program tumishi, simu za mkononi na kompyuta’’ imeeleza sehemu ya tenda hiyo.
Pia masharti ya tenda hiyo yameeleza kumruhusu mfanyakazi wa basi kumkatia tiketi mteja sambamba na wakala wa basi hilo kuweza kufanya hivyo au kwa mteja wenyewe kuweza kukata tiketi hiyo.
Zinazohusiana:
- Serikali inavyoangazia daladala, mabasi ya mikoani kuongeza mapato kielektroniki
- Taboa wazungumzia agizo la Lugola kuruhusu mabasi kusafiri saa 24
Huku mfumo huo ukitakiwa kuhakikisha unaweza kuthibiti kwa kukata tiketi moja kwa mtu mmoja na kuweza kuunganisha na mifumo ya risiti ya Mamlaka ya mapato Tanzania ( EFD machine).
Katibu mkuu wa Taboa, Enea Mrutu ameaiambia www.nukta.co.tz amesema kupitia mfumo huo, msafiri ataweza kukata tekiti muda wowote huku akisema mradi huo utaanza kwa majaribio katika baadhi ya mikoa ambayo itagawanywa katika kanda.
Mwisho wa kuomba tenda hiyo ni Februari 22 ,2020.
Hii inaweza kuwa fursa muhimu kwa vijana wabunifu kutumia ujuzi wa teknolojia walionao kuwarahisishia maisha watumiaji wa vyombo vya moto hasa wanaosafiri kwenda mikoani.
Latest