Jifunze nguvu ya familia katika filamu ya “Coffee and Kareem”

June 12, 2020 10:30 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayomhusu kijana mwenye miaka 12 anayetaka kutenganisha penzi la mama yake na mpenzi wake mpya.
  • Safari yake inamfanya kuwa shuhuda wa mauaji na anaishia kuwa “panya kwenye nyumba ya paka”.
  • Kiitikio cha filamu hii ni baada ya familia nzima kulazimika kukaa pamoja. Wataweza?

Dar es Salaam. Hata kabla ya jua kuchomoza, Kareem anamfuma mama yake na mpenzi wake wakiwa kwenye tendo la kuujaza ulimwengu. Ni tendo gani? Najua umeelewa!

Kijana huyo mwenye miaka 12 ambaye anaishi na mama yake pekee, hakufurahishwa na kitendo cha mama yake kuwa na mwanamume mwingine. 

Hapo ndipo safari ya kuhakikisha uhusiano wa polisi James Coffee (Ed Helms) na mama yake Vanessa Manning (Taraji Henson) unafikia ukingoni.

Kareem anatafuta kundi maalum la kumpatia Coffee kipigo cha mbwa koko ili aachane na mama yake. Akiwa katika safari hiyo, anaona yasiyopaswa kuonekana.

Lahaula! Kitumbua kimeingia mchanga kwani Kareem ameshuhudia mauaji na ni shahidi anayetafutwa na kundi la nguli wa kuuza madawa ya kulevya kwenye mji wa Detroit nchini Marekani. 

Sio yeye tu, ni Kareem na Coffee wanaotafutwa na genge la wahalifu wakiwemo Rodney (King Bach) na Orlando Johnson (RonReaco Lee).


Zinazohusiana


Hali inazidi kuwa mbaya baada ya mama kuingia kwenye mchezo huo wa paka na panya unaolazimu watatu hao kukaa pamoja.

Unahitaji kuvunja mbavu wikiendi hii, mwachie hiyo kazi Kareem na wazazi wake kwenye filamu ya “Kareem and Cofee” inayopatikana katika mtandao wa Netflix.

Umelipia kifurushi chako? Usisahau kukitumia kwa kutazama filamu hii ya muda wa saa 1:28.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV