Ahueni, maumivu: Bei ya mchele ikipanda Dodoma

September 7, 2020 1:04 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya jumla ya zao hilo imepanda kwa Sh55,000 ndani ya kipindi cha wiki moja. 
  • Itakuwa kicheko kwa wafanyabiashara na maumivu kwa wanunuzi. 

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa mchele katika jiji la Dodoma leo watalala na tabasamu baada ya bei ya jumla ya zao hilo kupanda kwa Sh55,000 ndani ya kipindi cha wiki moja. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (September 7, 2020) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo linauzwa kwa Sh220,000 katika soko la Majengo jijini humo ikiwa imepanda kutoka Sh165,000 iliyorekodiwa Jumatatu Agosti 31, 2020.

Hiyo ni sawa na kusema wafanyabiashara hao wataweka kibindoni Sh55,000 kwa kila gunia moja la mchele wanalouza leo sokoni. 

​Pia takwimu hizo ambazo hutolewa mara tatu kwa wiki, zinaonyesha kuwa bei ya chini ya mchele jijini humo imepanda hadi Sh160,000 kutoka Sh110,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita katika soko hilo hilo la Majengo. 

Kwa bei hizo zinazotumika leo, itakuwa ni maumivu kwa wanunuzi na kicheko kwa wafanyabiashara ambao kupanda kwa bei za mazao ndiyo faida kwao. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV