Uzushi: Kushiriki ngono mara kwa mara hakuzuii Corona
- Njia sahihi ya kujilinda dhidi ya Corona ni kuvaa barakoa, kunawa mikono na kukaa umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine.
- Ngono inaongeza uwezekano wa kupata Corona kuliko kuzuia.
Dar es Salaam. Kama ni miongoni mwa watu ambao wamekutana na habari mtandaoni inayohamasisha watu kushiriki ngono mara kwa mara ili kujikinga na Corona, fahamu wazi kuwa unadanganywa kwa sababu hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu dhana hiyo.
Kwa sasa katika mitandao ya kijamii hasa WhatsApp inasambaa picha yenye maneno yanayodai kuwa dawa ya virusi vya Corona imegunduliwa ambapo watu wanatakiwa kufanya mapenzi mara kwa mara ili kujikinga na ugonjwa huo, jambo si la kweli.
Habari picha hiyo ni uzushi unaolenga kupotosha watu.
Habari hiyo yenye picha ya Mtangazaji wa Shirika Habari la CNN la Marekani Wold Blitzer inaonyesha sehemu ya habari mpasuko (Breaking News) ikiwa na maelezo kwa lugha ya Kiengereza kuwa “constant sex kills coronavirus” ikimanisha kuwa “kufanya mapenzi mara kwa mara kunaua virusi vya Corona”.

Mpaka sasa hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha madai hayo. Mamlaka za afya likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) halijatoa tamko lolote kuhusu dhana hiyo, zaidi ya kuwataka watu kuchukua tahadhari zinazopendekezwa na wataalam wa afya ikiwemo kuvaa barakoa.
Tahadhari nyingine ni kukaa umbali mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine.
Katika kipindi ambacho Corona imeleta taharuki duniani, ni vema kupata taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo kutoka katika vyanzo sahihi ikiwemo WHO ili kujiweka salama zaidi.
Latest