Simbachawene: Imarisheni ulinzi wa sungusungu

May 17, 2021 1:15 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema vikundi hivyo vitasaidia kupunguza uhalifu kwenye jamii.

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya ndani, George  Simbachewe  ameagiza kuimarishwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi vikiwemo vya sungusungu ili kudhibiti vitendo vya kihalifu na wizi mdogo mdogo unatokea kwenye jamii. 

Agizo hilo la Simbachawene linaweza kuwa ni utekelezaji wa agizo la  Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizungumza na Wazee jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Mei 7, 2021) kuwa Jeshi la Polisi na jamii idhibiti tabia za wizi, uporaji na ujambazi ambazo zimeanza kuibuka tena hasa katika majiji makubwa likiwemo la Dar es Salaam.

Akizungumza leo Mei 17, 2021 jijini Mwanza alipofanya ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali vya Jeshi la Polisi likiwemo dawati la jinsia, uhamiaji na Gereza la Butimba,  Waziri Simbachawebe ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa polisi ambao umesaidia kupunguza uhalifu majini na nchi kavu. 

Hata hivyo, amesema jeshi hilo linapaswa kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao kwa kuhakikisha sungusungu wanafanya kazi zao vizuri kwenye mitaa mbalimbali ili kutokomeza uhalifu wa kila namna. 


Soma zaidi: 


“Tunatambua kuwepo kwa changamoto nyingi za uhalifu ndani ya Ziwa na kama hakuna boti la kusaidia katika kupambana inaweza kuongeza uhalifu  hivyo  ni vema boti litengenezwe na gharama zitumwe haraka,” amesema Waziri huyo wakati alipotembelea kikosi ya majini jijini hapa. 

Mbali na kitengo hicho pia Waziri huyo ametembele kikosi cha Jeshi la Zimamoto na  kuagiza kufanyika uchunguzi wa kina kwa matukio ya moto mashuleni na kueleza kuwa mengi hufanywa kwa hujuma za wanafunzi. 

“Ninaagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kwenye matukio ya moto mashuleni ambapo mengi yamebainika kufanywa na wanafunzi kwa utundu wao na wenye lengo la kuhujumu,  matukio haya yachunguzwe na yapatiwe suluhu na si kuishia hewani, ” amesisitiza. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi 2026-27

Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi 2026-27

Nukta TV

Waziri Khamis: Serikali haijaongeza kodi kwa bodaboda

Waziri Khamis: Serikali haijaongeza kodi kwa bodaboda

Nukta TV

Nyavu za samaki zamuibua Ado Shaibu bungeni, Spika Zungu amtuliza

Nyavu za samaki zamuibua Ado Shaibu bungeni, Spika Zungu amtuliza

Nukta TV