Filamu: “Uongo” unapobaki tumaini la kuukomboa ulimwengu

June 18, 2021 12:31 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayomhusu mungu wa utundu na udanganyifu.
  • Loki ambaye mecheza na mpangilio wa muda analazimika kulipia makosa yake.
  • Imani ya mamlaka za kutoa haki juu ya Loki bado ipo kwenye kitendawili.

Ni vigumu kumuamini mtu ambaye hawezi kusimamia maneno yake. Mfano akikupatia ahadi ya kuwa atafanya jambo fulani na kisha asifanye, lazima itakuwa ni ngumu kwa wewe kuamini pale atakapotoa ahadi nyingine kwako.

Hata hivyo, kuna wakati hufika ambapo mtu huyo ndiye mtu pekee anayeweza kuwa na msaada kwako. Utachagua nini? Kuteketea au kuipa imani yako juu yake nafasi nyingine?

Hali ndiyo ilikuwa hivyo kwa Loki ambaye ni mungu wa utundu na udanganyifu katika dunia ya kufikirika. Unaweza kumkumbuka Loki kupitia filamu za “Avengers” na “Thor” ambapo ameigiza kama mdogo wake na Thor.

Katika filamu ya muendelezo ya “Loki” mungu huyo anafanikiwa kutoroka kwa kutumia kidani (tesseract) ambacho kina uwezo wa kumsafirisha aliyenacho katika muda wowote yaani wakati uliopita, ujao na hata kuona kesho. 

Katika safari hiyo, Loki anashindwa kutumia muda wake vizuri. Hata ungekuwa wewe umepata nafasi ya kusafiri katika muda, kuna mambo ambayo utatamani uyabadili ikiwemo kucheza na siku yako ya kupatwa na mabaya au hata kujizuia usipate ajali itakayosababisha kifo.

                     

Katika kufanya hivyo, ni lazima utaathiri mipango ya mbingu na kusababisha yasiyoeleweka. Hicho ndicho alichokifanya Loki.

Inawadia siku ambayo mungu huyo wa uongo  na utundu inabidi alipie hesabu ya maneno yake ya udanganyifu lakini wakati huo ulimwengu nao unapanga mambo yake yanayomuacha Loki kuwa msaada pekee kwa usalama wa ulimwengu.

Mamlaka zinazomshikilia zina machaguo mawili: kumwacha Loki achape kazi ya kurekebisha makosa yake au ziendelee kumshikilia ili alipie makosa yake huku ulimwengu ukiteketea.

Unahisi watafanya nini ikiwa Loki ndiye mtu pekee anayeweza kuuokoa ulimwengu japo kuamini hata hatua yake moja ni sawa na kuamini fisi mwenye njaa akulindie bucha?

Fuatilia filamu hii ya muendelezo inayopatikana katika jukwaa la filamu la DisneyPlus pamoja na majukwaa mengine ya mtandaoni ikiwemo Amazon, Hulu na ESPN.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV