Nusu ya watoto wanaougua saratani hufariki dunia Afrika

August 17, 2021 11:17 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwaka 2020 kulikuwa na wagonjwa  wa saratani watoto wapatao 52,000.
  • kati yao zaidi ya nusu walifariki dunia.
  • Vifo hivyo vilichngiwa na athari za ugonjwa wa Corona.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema watoto wanaougua saratani barani Afrika wako hatarini kupoteza maisha hivi sasa kutokana na kushuka kwa huduma za matibabu za saratani katika kipindi cha janga la Corona au COVID-19.

Mratibu wa programu ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa  kanda ya Afrika wa WHO, Jean Marie Dangou amesema mwaka 2020 kulikuwa na wagonjwa  wa saratani watoto wapatao 52,000 kati yao zaidi ya nusu walifariki dunia .

“Tunakadiria kwamba zaidi ya watoto 28,000 walikufa kwa saratani au kansa katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Hii inavunja moyo sana kwa kuwa saratani ya utotoni inatibika ikibainika mapema na mgonjwa kupatiwa tiba stahiki,” amesema Dangou Agosti 13 mwaka huu wakati akitoa taarifa kuhusu ugonjwa huo.

Amesema ili kuokoa maisha ya watoto zinahitajika juhudi za makusudi za uwekezaji za miundombinu na matibabu ya watu wa bara hilo.

Pia amesisitiza  uwekezaji mahususi kwenye kukinga na kutibu kansa ikiwemo kutoa mafunzo ya hali ya juu kwa watoa huduma kwa lengo la kupunguza vifo na idadi ya wagonjwa.

Kila mtu binafsi anawajibika kuchukua juhudi za makusudi za kujielewesha vyema kuhusu saratani ya watoto na dalili za hatari ili kuweza kuongeza ugunduzi wa mapema na kupatiwa matibabu,” amesema  Dkt Dangou.

Sababu za kushuka kwa huduma za matibabu za saratani katika kipindi cha janga la Corona au COVID-19 ni pamoja na uchache wa watoa huduma za afya ambao wengi walijikita kuhudumia wagonjwa wa Corona.

Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa asilimia 72 ya nchi za Afrika zilikuwa na upungufu wa watoa huduma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV