Mambo ya kuzingatia kwa makundi haya kabla ya kuchanjwa chanjo ya Uviko-19

August 17, 2021 11:31 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni watu wenye mzio wa baadhi ya vitu au dawa.
  • Watu wenye magonjwa sugu.
  • Wanashauriwa kumuona daktari kabla ya kupata chanjo.

Dar es Salaam. Wakati nchi mbalimbali duniani zikiendelea kutoa chanjo ya Corona kwa wananchi wake, ni muhimu kujua vigezo au makundi ya watu wanaoruhusiwa kupata chanjo zilizoidhinishwa kama nyenzo muhimu ya kuimarisha kinga dhidi ya maambukizi ya Uviko-19.

Shirika la Afya Duniani (WHO) katika mwongozo wake wa utoaji chanjo imetaja makundi ya watu wasioruhusiwa kupata chanjo ya Uviko-19 mpaka  bila ushauri wa daktari. Makundi hayo ni:  

Watu walio na umri chini ya miaka 18 

Kwa mujibu wa WHO hiyo, kwa sasa watoto walio chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kupata chanjo.

Shirika hilo limeeleza kuwa tafiti zaidi zinahitajika  ili kujiridhisha iwapo watoto chini ya miaka 18 wanaruhusiwa kupata chanjo ya Corona tofauti na watu wazima ambao walikua sehemu ya tafiti zilizofanywa na wataalamu. 

“Ushahidi wa kutosha unahitajika ili kuruhusu matumizi ya chanjo mbalimbali za Corona kwa watoto,” inasomeka sehemu ya mwongozo huo.

Kabla ya kuamua kupata chanjo wanashauriwa kumwona daktari. Picha | John Hopkines Medicine

Watu wenye magonjwa ya kuambukiza

Watu wenye matatizo ya magonjwa sugu kama kisukari, pumu, shinikizo la damu au wenye matatizo ya kinga ndogo ya mwili wanashauriwa kutembelea kituo cha afya na kuonana na daktari kabla ya kuchukua uamuzi wa kupata chanjo ya Uviko-19.

Ushauri wa daktari ni muhimu ili kuepusha madhara anayoweza kupata mtu ikiwemo kifo.


Watu wenye mzio (allegy) 

Dk Arkan Ibwe kutoka programu ya Marekani ya U.S Peace Corps wakati akiongea katika mkutano uliolenga kutoa ufafanuzi juu ya chanjo ya Johnson & Johnson na wanahabari Agosti 5, 2021 alisema inashauriwa mtu mwenye mzio naye anatakiwa kumuona daktari kabla hajapata chanjo.

Hiyo itasaidia kufahamu kama chanjo husika inaendana na hali yake ya mwili. Huenda baadhi ya kemikali zilizopo kwenye chanjo hazishabihiani na mwili wake. Hivyo ushauri ni muhimu.

“Hizi chanjo ni muhimu ila kama mtu ana aleji na dawa ya aina yoyote ni muhimu asome vilivyopo kwenye chanjo au atembelee kituo kinachotoa chanjo aambiwe kama chanjo husika inamfaa,” alisema Dk Ibwe.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW