Serikali yatenga Sh15 bilioni kununua mahindi ya wakulima

September 2, 2021 3:20 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Hatua hiyo italeta ahueni kwa wakulima wenye hifadhi kubwa.
  • Serikali imefungua milango ya kuuza mahindi nje ya nchi.

Dar es salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa Sh15 bilioni kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

Hatua hiyo inaweza kuwapa ahueni wakulima ambao wamekuwa na malalamiko ya kuwa na mahindi mengi yaliyokosa soko na hivyo kuwaweka katika hatari ya kupata hasara.

Majaliwa ametoa kauli hiyo Septemba 2, 2021 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwela, Deus Sangu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

 “Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula (NFRA) tumeipa fedha za kwenda kununua mahindi kwa bei ya kumuwezesha mkulima ili ajikimu hadi msimu ujao. Uwezo si mkubwa sana, lakini tumeipa Sh15 bilioni,” amesema Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amesema alipokuwa ziarani mkoani Katavi aliona hali halisi ya mlundikano wa mahindi na akakutana na watu wa NFRA ili aone kasi ya ununuzi ikoje.

“Nilibaini kuwa uwezo wao ni mdogo na nikapokea malalamiko ya wananchi kwamba kituo cha kupokelea mahindi kiko mbali, kwa hiyo tumeamua kuanzia sasa kila halmashauri itapaswa iwe na kituo japo kimoja cha kupokelea mahindi ili kuharakisha ununuzi wa zao hilo,” amesema Majaliwa.

Amewahakikishia wakulima kuwa Serikali itanunua mahindi kupitia NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko na kuwa kuwa Serikali imefungua milango kwa yeyote anayetaka kuuza mahindi nje ya nchi. 

Mei 2021, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alitolea ufafanuzi wa suala la kununua mahindi kwa wakulima na aliainisha kuwa kwa wakati huo NFRA haikuwa na uwezo wa kununua mahindi ya wakulima lakini ipo mikakati inayofanyika kufungua soko la zao hilo nje ya nchi.

Hatua hiyo ya Serikali huenda ikawapa ahueni wakulima ambao wan a akiba kubwa ya mahindi kwenye maghala.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV