Tahadhari: Kirusi kipya cha Corona
November 29, 2021 12:10 pm ·
Herimina
- Ni kirusi cha Omicron, chenye uwezo wa kusambaa haraka.
- Wananchi watakiwa kuendelea kuchukua tahadhari.
Dar es salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO), Novemba 26, 2021 liliripoti uwepo wa aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 kiitwacho “Omicron”, kinachosemekana kuwa na uwezo wa kusambaa haraka.
Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Afya Tanzania imetoa tahadhari kwa Watanzania kuendelea kufuata ushauri wa wataalam wa afya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Hatua hizo ni pamoja na kuchanja chanjo ya Uviko-19 ambazo zinatolewa bure kwenye vituo vya afya na kuepuka sehemu zenye mikusanyiko ya watu.
Vile vile, uvaaji barakoa, kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka.

Latest
7 days ago
·
Lucy Samson
Vita ya Mashariki ya Kati yazidi kupaisha bei ya petroli, dizeli Tanzania
1 week ago
·
Kelvin Makwinya
Viwango vya kubadili fedha Machi 31, 2026
1 week ago
·
Lucy Samson
ATCL yaripoti hasara ya Sh191.1 bilioni, CAG aanika sababu
1 week ago
·
Kelvin Makwinya
Rais Samia apokea ripoti CAG, TAKUKURU na PPRA aagiza utekelezaji wa haraka
