Tanzania itakavyookoa mabilioni ujenzi wa kiwanda cha chanjo

February 16, 2022 8:25 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara yake rasmi nchini Ubelgiji. Picha| Ikulu.


  • Ni zaidi ya Sh26.1 bilioni zinazotumika kununua chanjo.
  • Pia itaimarisha mapambano dhidi ya Uviko-19.
  • Serikali yaanza mipango kujenga kiwanda hicho nchini.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema hadi kufikia mwaka 2030 itatumia Sh216 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya kununua chanjo za magonjwa mbalimbali ikiwemo ya Corona (Uviko-19). 

Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kimeongezeka kutoka Sh26.1 bilioni iliyokuwa inatumika mwaka 2020 kwa ajili ya kununua chanjo.

Asilimia kubwa ya chanjo hizo huagizwa nje ya nchi kutokana na Tanzania kuwa na viwanda vichache vya kutengeza dawa muhimu za binadamu. 

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, katika bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 ilitenga Sh63.2 bilioni kwa ajili ya ununuzi na usambazaji wa chanjo katika maeneo mbalimbali nchini.

Huduma za chanjo zilizoboreshwa husaidia kuwakinga watoto chini ya miaka 5, akina mama wajawazito huku chanjo nyingine za kimkakati hutumika kukinga na kudhibiti magonjwa yanayozuilika kama homa ya ini, kichaa cha mbwa na mengineyo.

Pia chanjo hupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi.


Soma zaidi:


Huenda Tanzania isiendelee kununua chanjo nje ya nchi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kudokeza kuwa Serikali yake inakusudia kujenga kiwanda cha chanjo nchini. 

Kiongozi huyo mkuu wa nchi aamewasilisha mpango huo wa Serikali mbele ya Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU) Charles Michael katika akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Ubelgiji.

Licha ya kuwa Rais hajasema gharama za mradi huo na sehemu kitakapojengwa kiwanda hicho, lakini kitapunguza gharama za ununuzi wa chanjo kwa Serikali na utaongeza urahisi wa upatikanaji wa chanjo nchini.

Pia kiwanda hicho kitafungua fursa za ajira kwa watalaam wa afya nchini kuendeleza ujuzi wao katika fani ya utabibu.

Kiwanda hicho pia kitakuwa kinatengeneza chanjo ya Uviko-19 ambayo imekuwa ikihitajika katika maeneo mbalimbali duniani.

Tanzania itaungana na nchi nyingine za Afrika ikiwemo Rwanda na Afrika Kusini ambazo zimeanza kujenga viwanda vya chanjo ya ugonjwa huo katika nchi zao. 

Novemba mwaka 2021, Rais Samia alipokutana na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni Ikulu jijini Dar es Salaa alidokeza kuwa nchi hizo mbili zitashirikiana katika ujenzi wa kiwanda cha chanjo.

“Tunataka wataalam wetu wakae wajadiliane  tunakwenda vipi kwenye kiwanda hicho,” alisema Rais Samia.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV