Maumivu, kicheko: Ewura ikitangaza bei mpya za petroli, dizeli

December 7, 2022 11:40 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya rejareja ya petroli yanayoingia kupitia Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zimepungua.
  • Bei ya dizeli yapanda kwa viwango tofauti.
  • Serikali yaondoa ruzuku kwa petroli inayoingia bandari ya Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Huenda itakuwa kicheko na maumivu kwa watumiaji wa nishati ya mafuta baada ya kutolewa kwa bei mpya zinazoonyesha kupanda na kushuka kwa petroli na dizeli kwa Disemba 2022. 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa hapa nchini ambazo zimeanza kutumika leo Desemba 7 2022.

Bei ya mafuta ya rejareja ya petroli yanayoingia kupitia bandari za Dar es Salaam na Mtwara imepungua kwa Sh59 kwa lita na Sh92 kwa lita, mtawalia, ikilinganishwa na bei za Novemba 2022.

Hiyo ina maana kuwa petroli kwa upande wa Dar es Salaam imeshuka hadi kufikia Sh2,827 kutoka Sh2,886 iliyokuwapo Novemba.

Kwa bei hiyo ya Disemba, mmiliki mwenye gari, akiwa na Sh10,000 atapata lita 3.5 za petroli ikilinganishwa na lita 3.4 alizokuwa akipata Novemba.  

Wenzao wa Mtwara wao watanunua petroli kwa Sh2,825 kwa lita kutoka Sh2,917 huku bei ya Tanga ikiongezeka kwa Sh9 kwa lita ikilinganishwa na bei ya mwezi uliopita.


Soma zaidi:


Kulingana na ukomo wa bei ya mafuta iliyokuwapo Novemba mwaka huu, bei ya petroli kwa upande wa Tanga imefikia Sh2,815 kutoka Sh2,806. 

“Hata hivyo, ili kuendelea kupunguza athari za ongezeko la bei za mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea dizeli, Serikali imetoa ruzuku kwa bei za Desemba 2022,” imeeleza Ewura, licha ya kuwa mafuta ya petroli kwa bandari ya Dar es Salaam hayana ruzuku.

“Kutokana na ruzuku hiyo, bei ya mafuta ya dizeli imepungua kwa Sh83 kwa lita, Sh247 na Sh243 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Kutokana na ruzuku hiyo, dizeli inauzwa kwa Sh3,247 kutoka Sh3,052 ya Novemba mwaka huu kwa upande wa Dar es Salaam huku wakazi wa Tanga wakinunua Dizeli kwa Sh3,496 kutoka Sh3,249 na Mtwara kwa Sh3,512 kutoka Sh3,269

“Bei ya mafuta ya taa kwa bandari ya Dar es salaam imeongezeka kwa Sh141 kwa lita ukilinganisha na bei zilizopita kwa sababu ya wastani wa bei kubwa zaidi ya mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia na gharama za usafirishaji,” imeeleza Ewura.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV