Serikali kukusanya zaidi ya Sh250 bilioni maduhuli ya ardhi kidijitali

July 14, 2022 11:08 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Fedha hizo zitatokana na kupima viwanja na kutoa hati.
  • Hati miliki 2.4 milioni za ardhi kutolewa kwa wananchi.

Mwanza. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatarajia kukusanya zaidi ya Sh250.1 bilioni kutokana na maduhuli ya sekta ya ardhi kwa kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kupima viwanja na kutoa hati miliki.

Njia itakayotumika kukusanya fedha hizo ni kwa kutumia mifumo ya kidijitali.

Miongoni mwa vipaumbele vitakavyosaidia kukusanya maduhuli hayo ni pamoja na kutoa hati miliki 2.4 milioni kwa wananchi ambao watapimiwa maeneo yao na kwamba hadi mpaka sasa hati hizo zimeshaandaliwa.

Mabula ametoa ufafanuzi huo Julai 12, 2022 kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Mwanza uliolenga kutoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2022/23.


Soma zaidi:


Dk Mabula amesema hadi sasa zaidi ya hati 24,000 nchi nzima za watu ambao wamekamilisha kulipia zimeshakamilika kwenye ofisi za wasajili lakini hawajaenda kuzichukua huku akieleza wasiwasi wake kuwa ni kutokana na uelewa wa kutosha wa watu kupata hati hizo.

“Changamoto iliyopo ni baadhi ya wananchi kushindwa kulipia hati hizo baada ya kupimiwa, takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 900,000 nchi nzima wameshapimiwa lakini hawajalipia kupata hati zao,” amesema Mabula.

Amesema kutokana na changamoto hiyo mwaka jana walipitisha sheria kila mwenye kiwanja kipimwe na kuanza kulipiwa kodi na hii haijalishi kama kina hati au hakina jambo ambalo linatekelezeka.

Aidha, Mabula amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kwenye suala la urasimishaji wa makazi ili kupunguza migogoro ya ardhi.

Amesema zoezi hilo lililoanza mwaka 2015 linatarajiwa kukamilika mwaka 2023 na kwamba kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya wananchi kutoshiriki katika zoezi hilo ili maeneo yao yaweze kutambuliwa.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV